2 Pallas

asteroidi

2 Pallas (au Palasi; alama: ⚴) ni asteroidi ya pili iliyowahi kutambuliwa katika Mfumo wa Jua. Iligunduliwa na mtibabu na mwanaastronomia Mjerumani Heinrich Wilhelm Matthäus Olbers mnamo 28 Machi 1802.[1]

Picha ya Pallas kwa rangi ya Urujuanimno

Jina la "2 Pallas" inaunganisha jina lililotolewa na Olbers, pamoja na namba ya asteroidi iliyojulikana. Jina lenyewe limanrejelea Pallas Athena aliyeabudiwa kama mungu katika dini ya Ugirki ya Kale.[2]

2 Pallas ina masi inayokadiriwa kuwa asilimia 7% ya masi yaote ya ukanda wa asteroidi. [3] Ni asteroidi kubwa ya tatu kulingana na masi yake, na ya pili kwa kuangalia kipenyo chake. Umbo lake linafanana na duaradufu yenye vipenyo kati ya km 500 na km 582.

References hariri

  1. "JPL Small-Body Database Browser". ssd.jpl.nasa.gov. 2011 [last update]. Iliwekwa mnamo March 21, 2011.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  2. Schmadel, Lutz D. (2003). Dictionary of minor planet names, Volume 1. Springer. uk. 15. ISBN 3540002383. Iliwekwa mnamo March 21, 2011.  Check date values in: |accessdate= (help)
  3. Pitjeva, E. V. (2005). "High-Precision Ephemerides of Planets—EPM and Determination of Some Astronomical Constants" (PDF). Solar System Research 39 (3): 176. doi:10.1007/s11208-005-0033-2. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-09-07. Iliwekwa mnamo 2021-02-14.