Ahmed Ben Bella (26 Desemba 1916 - 11 Aprili 2012) alikuwa mwanasiasa, mwanajeshi na mwanamapinduzi wa kisoshalisti wa Algeria ambaye aliwahi kuwa mkuu wa serikali kuanzia tarehe 27 Septemba 1962 hadi 15 Septemba 1963 na kisha Rais wa kwanza wa Algeria kutoka 15 Septemba 1963 hadi 19 Juni 1965.

Ahmed Ben Bella

Raisi Ahmed Ben Bella
Amekufa 11 Aprili 2012
Nchi Algeria
Kazi yake Mwanasiasa

Maisha Ya Awali hariri

Ahmed Ben Bella alizaliwa tarehe 26 Desemba 1916 katika wilaya ya Maghnia. Wazazi wake walikuwa wahamiaji kutoka Morocco. [1]

Utumishi na Jeshi la Ufaransa hariri

Ben Bella alijitolea kwa mara ya kwanza kutumika katika Jeshi la Ufaransa mwaka 1936. Jeshi lilikuwa mojawapo ya njia chache za maendeleo kwa Algeria chini ya utawala wa kikoloni na uandikishaji wa hiari ulikuwa wa kawaida. Alipotumwa kwenda nchi Marseille, alicheza kiungo wa kati wa klabu ya Olympique de Marseille mnamo 1939-1940. [2]

Marejeo hariri

  1. "Mort de Ben Bella, héros de l'indépendance algérienne", Le Monde.fr, 2012-04-11. (fr) 
  2. "Ben Bella profile on om-passion, unofficial Olympique de Marseille site". Om-passion.com. 24 October 2011. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 February 2009. Iliwekwa mnamo 12 April 2012.  More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help); More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); Check date values in: |date=, |archivedate=, |accessdate= (help)

Viungo Vya Nje hariri

  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ahmed Ben Bella kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.