Alexander Graham Bell

Alexander Graham Bell (3 Machi 18472 Agosti 1922) alikuwa kati ya wagunduzi wa mawasiliano ya simu. Alizaliwa katika mji wa Edinburgh nchini Uskoti lakini baadaye alihamia nchi za Kanada na Marekani. Baba yake alikuwa mwalimu wa watoto wenye matatizo ya kusikia na kuongea. Alifanikiwa katika jaribio lake la kwanza mwaka 1876.[1]

Alexander Graham Bell

Bell hakuwa mtu wa kwanza wa kutengeneza simu kwa mawasiliano lakini mashine yake ilikuwa ya kwanza iliyoweza kutumiwa kibiashara nje ya majaribio na maabara. Alitumia matokeo ya utafiti wa watangulizi hasa Mwitalia Antonio Meucci.

Marejeo hariri

  1. "Alexander Graham Bell Laboratory Notebook, 1875-1876". World Digital Library. 1875-1876. Iliwekwa mnamo 2013-07-23.  Check date values in: |date= (help)