Alhaji (Ar. الحاجّ; pia: hujaji) au hajja kwa wanawake ni neno la kumtaja Mwislamu aliyetimiza safari ya hajj. Haikubaliki kwa mtu yeyote aliyefika Makka lakini kwa hao pekee waliofanya hija hii wakati wa siku maalumu kwenye mwezi wa Dhul-hijja na kutekeleza ibada zote zinazotakiwa.

Alhaji hutumiwa pia kama cheo cha heshima na kuwa kama sehemu ya jina la mtu.

Matumizi nje ya Uislamu hariri

Neno latokea pia katika lugha kadhaa zilizoathiriwa na utamaduni wa Kiislamu kama sehemu ya majina ya watu wasio Waislamu. Kuna Wagiriki na Wabulgaria wengi wenye Χατζής (Khatzís) kwa Kigiriki na Хаджи (Khadji) au Хаджия (Khadjiya - ya kike) kwa Kibulgaria kama sehemu ya majina ya familia yao. Hii ni dalili ya kwamba babu fulani wa ukoo huu alifanya hija ya kwenda Yerusalemu penye mahali patakatifu pa Ukristo.

Jina kama hili linatokea kwa mfano kama Иван Хаджипетров yaani "Ivan Khadjipetrov".

Kuna matumizi ya kulingana kati ya Wayahudi wa Uajemi. Myahudi wa kule aliyefika Yerusalemu na kusali mbele ya ukuta wa maombolezo huitwa pia "haji"

Marejeo hariri