Ali Muhsin al-Barwani

Ali Muhsin Al-Barwani (13 Januari 1919 katika Mji Mkongwe - 20 Machi 2006 katika mji mkuu wa Muskat (Omani)) alikuwa mwanasiasa, mwanadiplomasia, na mshairi kutoka nchi ya Zanzibar chini ya Usultani wa Zanzibar. Alikuwa Waziri wa mambo ya nje wakati wa mamlaka ya Kiarabu baada ya Zanzibar kupata uhuru kutoka kwa mkoloni Muingereza na kabla ya Zanzibar kugeuka kuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Wasifu hariri

Maisha ya Sheikh hariri

Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani alikua mzalendo wa nchi ya Zanzibar ambae alipata mafunzo ya dini kwa baba yake Sheikh Muhsin bin Ali na kwa wanazuoni wengine pia wa Afrika ya Mashariki. Pia Sheikh Ali amesoma ilimu ya Kilimo Chuo Kikuu cha Makerere (Makerere University) huko Uganda.

Sheikh Ali alianza maisha yake kwa kufanya kazi ya kilimo na uwalimu. Katika mwaka 1947 Aliacha kazi ya serikali, ili ashughulikie jihadi ya nchi yake na Umma wake.

Kazi yake ya magazeti hariri

Sheikh Ali alikua Mhariri Mkuu wa gazeti la Mwongozi kwa muda wa miaka kumi na tano. Mwongozi lilikua gazeti la siasa na jamii na la dini, na lilikua maarufu gazeti hilo kwa kazi yake kubwa ya kudai haki za wananchi na kutapakaza misingi ya Kiislamu huko Zanzibar na sehemu mbali mbali za Afrika ya Mashariki

Kuongoza kwake Chama cha Hizbu hariri

Sheikh Ali Muhsin aliongoza chama cha Hizbu(Zanzibar Nationalist Party) na aliongoza jihadi ya Uhuru wa Zanzibar dhidi ya Muingereza. Hapo aliitwa Zaim na raia wa Zanzibar yaani zaim ni Kiongozi.

Kazi zake hariri

Sheikh Ali alitumika kazi mbali mbali huko Zanzibar alifanya kazi ya Waziri wa Ilimu na Waziri wa Mambo ya ndani, Baadae akapewa kazi ya Naibu wa Waziri mkuu, na Waziri wa Mambo ya nje katika serikali ya Kidemokrasia ya Zanzibar.

Serikali yake kupinduliwa hariri

Januari mwaka 1964, serikali yake ilipinduliwa mapinduzi hayo yalisababisha kumwagika kwa damu za watu wengi hadi ulimwengu ulishtuka kutokana na kumwagika damu hizo maana walikufa watu wengi sana, Sheikh Ali Muhsin aliwekwa jela kwa zaidi ya myaka kumi bila kushtakiwa kwa sababu ya fikra zake za kisiasa.

Kuachwa kwake hariri

Mwaka 1974 Sheikh Ali Muhsin alifunguliwa nakuachiwa huru, akaamua kuondoka nakuelekea Kenya nakuomba ukimbizi na wakati alipopata ukimbizi aliamua kuelekea Misri, Kairo, Alikaa muda mrefu huko Kairokiasi cha myaka 10 na huko alisoma katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar nchini Misri, yeye alikua rafiki mzuri wa raisi wa Misri Gamal Abdel Nasser. Baada ya kukaa muda mrefu huko Misri aliamua kurejea Kenya, na baadae aliamua kuelekea Falme za Kiarabu,Dubai na huko huko ndio alifasiri Qurani kwa Lugha ya Kiswahili ambayo inaumashuhuri mwingi kwa wale Waislamu wazungumzao Lugha ya Kiswahili ulimwenguni haswa Afrika ya Mashariki na ya Kati pia na ya Kusini na Visiwa vya bahari Hindi

Tungo zake kadhaa hariri

Ametunga Mashairi ya Kiswahili yenye beti 1300 Juu ya maisha ya mtume Muhammad (S.A.W) Ametunga kitabu cha Kiingereza cha Kulinganisha Ukristo na Uiislamu alikifasiri mwenyewe kwa lugha ya Kiswahili pia. Amefasiri Qurani tukufu kwa Lugha ya Kiswahili.("Al Muntakhab Fi Tafseer Al Qur'an".)

Kufa kwake hariri

Sheikh Ali Muhsin (Mungu amuweke mahala pema) aliiaga dunia siku ya Jumatatu mwezi wa Machi,2006, Alifariki akiwa na umri wa myaka 86.

Viungo vya nje hariri