Amir H. Jamal

Mwanasiasa wa Tanzania

Amir Habib Jamal (26 Januari 1922 - 21 Machi 1995) alikuwa mwanasiasa na mwanadiplomasia wa Tanzania ambaye aliwahi kuwa waziri enzi za utawala wa Mwalimu Julius Nyerere.[1][2] Aliwakilisha jimbo la Morogoro kuanzia mwaka 1960 hadi mwaka 1985.[3] na alikuwa Waziri wa fedha aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi kwani aliongoza wizara hiyo kwa takriban miaka 12.

Maisha ya awali hariri

Jamal alizaliwa na Wahindi walioishi Tanganyika, ambayo ni Tanzania leo.[4]. Alikuwa mtoto wa Kulsum Thawer na Habib Jamal, mwanachama mwanzilishi wa Chama cha Waasia. Alisoma katika mji wa Mwanza na akaenda kusoma elimu yake ya sekondari katika jiji la [Dar es Salaam]]. Alihitimu masomo ya juu katika Chuo Kikuu cha Calcutta nchini India katika fani ya uchumi bcom.[1]

Alikuwa na ndoto ya kufundisha kama daktari katika Chuo Kikuu cha Mumbay Lakini licha ya alama zake za juu, hakuingia katika kitivo cha matibabu.[5]. Mwaka 1942, Alihudhuria mkutano wa Bunge la Kitaifa la India ambapo Mahatma Gandhi alizindua harakati za kuiacha india, akidai uondoaji wa haraka wa Dola la Uingereza nchini India.[6] Baada ya kuhitimu, alirudi Dar es Salaam na kujiunga na biashara ya familia.[5]

Alikutana mara ya kwanza na Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1952 katika mapokezi ya Baraza la Uingereza kwa heshima ya kurudi baada ya kuhitimu katika Chuo Kikuu cha Edinburgh.[7] Alikuwa mzee wa harakati za uhuru wa Tanganyika, na mwaka wa 1955 alisaidia kulipa bili ya ziara ya Nyerere kwenda [[Umoja wa Mataifa] huko katika jiji la New York marekani.[8]

Picha hariri

Marejeo hariri

  1. 1.0 1.1 Europa Publications (2003). The International Who's Who 2004. Psychology Press. ku. 804–. ISBN 978-1-85743-217-6. 
  2. "Biography: Amir H. Jamal". Centre for Global Negotiations. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-07-25. Iliwekwa mnamo 3 March 2013.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); Check date values in: |accessdate= (help)
  3. "Amir Habib Jamal: A Tribute from Mwalimu J.K. Nyerere". Dag Hammarskjöld Foundation. 1995. uk. 95. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-07-25. Iliwekwa mnamo 25 July 2015.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); Check date values in: |accessdate= (help)
  4. Godfrey Mwakikagile (2006). Life Under Nyerere. Intercontinental Books. ku. 95–. ISBN 978-0-9802587-2-1. 
  5. 5.0 5.1 Judith Márffy-Mantuano Hare Countess of Listowel (1965). The Making of Tanganyika. Chatto & Windus. 
  6. Vassanji 2014, p. 327
  7. Colin Legum; G. R. V. Mmari (1 January 1995). Mwalimu: The Influence of Nyerere. James Currey Publishers. ku. 7–. ISBN 978-0-85255-386-2.  Check date values in: |date= (help)
  8. Ronald Aminzade (31 October 2013). Race, Nation, and Citizenship in Post-Colonial Africa: The Case of Tanzania. Cambridge University Press. ku. 108–. ISBN 978-1-107-04438-8.  Check date values in: |date= (help)