Anastasi wa Pavia
Anastasi wa Pavia (alifariki Pavia, Lombardia, Italia 680 BK) anakumbukwa kama askofu wa 17 wa mji huo wa Italia Kaskazini kuanzia mwaka 668 hivi hadi kifo chake.
Kabla ya hapo alikuwa askofu wa Pavia upande wa Waario, lakini alikanusha uzushi wao akashika kwa uimara imani ya Kikatoliki akipinga pia uzushi mpya kuhusu utashi wa Yesu Kristo[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Tazama pia hariri
Tanbihi hariri
Viungo vya nje hariri
- St. Anastasius XV Catholic Online
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |