Anibale Maria di Francia

Anibale Maria di Francia (Messina, Sicilia, Italia, 5 Julai 1851 – Messina, 1 Juni 1927) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki aliyeanzisha mashirika mawili ya kitawa ili kumuomba Mungu alijalie Kanisa lake lizae mapadri watakatifu wengi: Mapadri Warogasyonisti na Mabinti wa Ari ya Kimungu[1].

Sanamu ya Mt. Anibale Maria di Francia huko Bay, Laguna.

Pia alijenga nyumba kadhaa kwa ajili ya mayatima na kuwanyoshea fukara wote mikono yenye huruma ya Mungu[2].

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 7 Oktoba 1990 halafu mtakatifu tarehe 16 Mei 2004.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.