Mtakatifu Ansgar (Amiens, Ufaransa, labda 8 Septemba 801Bremen Ujerumani, 3 Februari 865) alikuwa askofu mmisionari kutoka Ufaransa.

Mt. Ansgari akiwahubiri Waswidi.

Tangu kale ametambuliwa kuwa mtakatifu.

Sikukuu yake ni 3 Februari[1].

Maisha hariri

Ansgar alijiunga na monasteri huko Corbie.

Mwaka 826 alikwenda kuhubiri Injili nchini Denmark, ambako hakufanikisha sana, hivyo akaenda Uswidi.

Alikuwa askofu wa Hamburg, halafu akaongezewaa Bremen pia, upande wa kaskazini wa Ujerumani. Ndipo alipofariki kutokana na uchovu wa kazi zake,Pia alikuwa balozi wa Papa Gregori IV katika Denmark na Uswidi.

Alivumilia magumu mengi sana katika kazi ya uenezaji Injili, asikate tamaa.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

  • Pryce, Mark. Literary Companion to the Festivals: A Poetic Gathering to Accompany Liturgical Celebrations of Commemorations and Festivals. Minneapolis: Fortress Press, 2003.
  • Tschan, Francis J. History of the Archbishops of Hamburg-Bremen. New York: Columbia University Press, 1959.
  • Wood, Ian. The Missionary Life: Saints and the Evangelisation of Europe, 400 – 1050. Great Britain: Longman, 2001.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.