Antoni Daniel, S.J. (Dieppe, Ufaransa 25 Mei 1601 – karibu na Teanaostaye, Kanada, 4 Julai 1648) alikuwa padri wa Wajesuiti mmisionari kwa Wahuroni wa Amerika Kaskazini tangu mwaka 1632[1].

Wajesuiti wafiadini wa Amerika Kaskazini.

Aliuawa kwa mishale na Wairoki, kabila lingine la Waindio, akisimama mlangoni mwa kanisa alipomaliza kuadhimisha Misa na akiwa na lengo la kulinda waumini wapya. Hatimaye alichomwa moto.

Alitangazwa na Papa Pius XI kuwa mwenye heri tarehe 21 Juni 1925, na kuwa mtakatifu tarehe 29 Juni 1930.

Sikukuu ya kundi lake la wafiadini huadhimishwa tarehe 19 Oktoba, lakini ya kwake mwenyewe huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

  • Rochemonteix, Les Jésuites et la Nouvelle-France au XVIIe siècle, I, 97–100, 409–18.
  • Attwater, Donald and Catherine Rachel John. The Penguin Dictionary of Saints. 3rd edition. New York: Penguin Books, 1993. ISBN 0-14-051312-4.

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.