Anzel Solomons

Mchezaji wa sataranji wa Africa kusini

Anzel Solomons ( née Laubscher, alizaliwa 6 Januari 1978) ni mchezaji wa chess wa Afrika Kusini. Alipokea jina katika FIDE la Woman International Master (WIM) mnamo mwaka 2003.

Kazi hariri

Alitunukiwa taji la Woman International Master kwa ushindi wake katika mashindano ya FIDE kanda ya Afrika nchini Botswana . Mnamo mwaka 2007, huko Windhoek, Anzel Solomons alishinda medali ya silva katika mashindano ya Afrika ya Chess ya Women's Chess Championship. [1] Mnamo 2008, huko Nalchik Anzel Solomons alishiriki katika mashindano ya Dunia ya Chess ya Women's World Chess Championship, ambapo alipoteza katika raundi ya kwanza kwa Xu Yuhua . [2] Mnamo 2011, alimaliza raundi 2 katika mashindano ya kimataifa ya wanawake ya mfumo wa Uswizi huko Luanda . [3] Mnamo 2014, Anzel Solomons alishinda medali yake ya pili ya silva katika mashindano ya Chess ya wanawake ya Afrika. [4]

Ameichezea Afrika Kusini katika mashindano saba za Chess ya wanawake (1998, [5] 2006-2016 [6] ) na katika mashindano ya dunia ya Chess ya timu ya wanawake (World Women's Team Chess Championship) mwaka 2011. [7] Anzel Solomons ameshiriki mara mbili katika mashindano ya timu ya Chess ya wanawake katika Michezo ya Afrika (2007-2011), na kushinda medali ya silva mnamo mwaka 2007, na medali ya shaba mnamo mwaka 2011. [8]

Marejeo hariri

  1. "The Week in Chess 671". TheWeekInChess.com. 
  2. "2008 FIDE Knockout Matches : World Chess Championship (women)". Mark-Weeks.com. 
  3. "FIDE Original Tournament Report". ratings.fide.com. 
  4. Herzog, Heinz. "African Individual Chess Championships 2014". Chess-Results.com. 
  5. Bartelski, Wojciech. "Women's Chess Olympiads :: Anzel Laubscher". OlimpBase.org. 
  6. Bartelski, Wojciech. "Women's Chess Olympiads :: Anzel Solomons". OlimpBase.org. 
  7. Bartelski, Wojciech. "World Women's Team Chess Championship :: Anzel Solomons". OlimpBase.org. 
  8. Bartelski, Wojciech. "All-Africa Games (chess - women) :: Anzel Solomons". OlimpBase.org.