Aramex (kwa Kiarabu: ارامكس ’arāmaks) ni kampuni ya kimataifa ya masuala ya usafirishaji na uwekaji katika ghala wa bidhaa, usafirishaji kwa njia ya ndege na usafirishaji wa mizigo ndani ya nchi mbalimbali. Kampuni hii ilianzishwa mwaka 1982 na makao yake makuu yako Amman, Jordan. Aramex pia inatoa huduma za reja reja kama vile usambazaji wa barua.

Aramex
Makao MakuuAmman, Jordan
Tovutiwww.aramex.com

Historia hariri

Aramex ilianzishwa na Fadi Ghandour mwaka 1982, ambapo jina lake lilifupishwa kutoka majina ya "ARab AMerica EXpress" na kutengeneza jina la Aramex. Mnamo mwaka 1982, Mr. Ghandour alianza kufanya kazi kama mfanyakazi wa mizigo midogo midogo kwenda Amerika ya Kaskazini katika makampuni ya kusafirisha mizigo kama vile FedEx, Purolator, Burlington Northern, Emery, na Airborne Express ikiwa na DHL kama mshindani wake mkubwa katika eneo hilo, pamoja na Airborne Express, kama mshirika wa shirika la usafirishaji la ulimwengu.

Kampuni hii iliyasaidia makampuni shirika yake ambayo yalikua madogo kuweza kushindana na makampuni makubwa.[1] Mwaka 1997, Aramex iliandikishwa katika soko la hisa la Marekani linalofahamika kama NASDAQ, na kampuni ya kwanza ya kimataifa kuweza kufaya hivyo. Mnamo mwaka 2002, wakati Aramex ikisherehekea kumbukumbu ya miaka 20, Abraaj Capital alipendekaza Aramex kujitoa katika soko la hisa la Marekani, na kuwa kampuni binafsi na hatiye Aramex ilijitoa katika soko hilo na kuwa kampuni binafsi. Hatimaye kampuni ilirejea katika umiliki binafsi baada ya utawala wa kampuni hiyo kuamua kuinunua, akiwamo mkurugenzi mkuu na mwanzilishi wake Fadi Gandour.[2]

Mnamo mwaka 2003, kampuni ya DHL ilinunua kampuni ya Airborne Express, kampuni iliyokuwa mshirika mkuu wa Aramex nchini Marekani. Hii ilisababisha kampuni ya Airborne kusitisha ushirika huo. Mwaka huu, kampuni ya Arames ilichukua nafasi hiyo huku ikipata ushirika kutoka kwa kampuni ya Global Distribution Alliance (GDA), kampuni inayofanyakazi ulimwengu mzima, ikishirikiana na mashirika 40 na kuwa na kiasi cha mtaji wa $7.5 billion.

Aramex inaongoza katika ushirikiano huu, na hasa hutumia mfumo wa Shipment management system ulionzishwa na kampuni hiyo.[3][4][5]

Baada ya kuamua kijiandikisha katika soko la hisa la Dubai, toleo la kwanza la kampuni kwa umma lilikua na jumla ya hisa 550 milioni zilizokuwa zikiuzwa kiasi cha Dirham 1 kwa kila hisa.[6]

Kama sehemu ya mpango wake wa kutaka kupanuka, Aramex iliongeza aina za huduma iliyokua ikitoa ikiwa ni pamoja na kuongeza huduma za Priority Airfreight, InfoFort, Freight Professionals and TwoWay-Vanguard.[7][8][9]

Mwandishi mkubwa wa kimataifa Thomas L. Friedman aliitumia kampuni ya Aramex katika kitabu chake cha The World Is Flat kama mfano wa makampuni ambayo yeye anayataja kuwa yamenufaika na mfumo wa dunia kuwa tambarare. Mfumo wa dunia kuwa tambarare ni ule usawa unaopatikana katika masuala ya uchumi baada kuondolewa kwa mipaka ya kijiografia na makampuni kuweza kutanuka na kusambaa katika maeneo mbalimbali duniani. Hii ikiwa ni pamoja na makampuni kuungana na kuzidisha ushindani.[10][11]

Marejeo hariri

  1. "Shuaa Capital Research". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-10-04. Iliwekwa mnamo 2011-12-10. 
  2. "Abraaj Capital". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-09-28. Iliwekwa mnamo 2011-12-10. 
  3. Friedman, Thomas (2006). The World is Flat. 
  4. "Abraaj Capital". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-10-20. Iliwekwa mnamo 2011-12-10. 
  5. "Global Distribution Alliance". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-05-14. Iliwekwa mnamo 2011-12-10. 
  6. "AIL board of directors approves the acquisition of Aramex from Abraaj". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-05-18. Iliwekwa mnamo 2011-12-10. 
  7. "InfoFort". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-10-23. Iliwekwa mnamo 2011-12-10. 
  8. "Priority Airfreight". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-05-18. Iliwekwa mnamo 2011-12-10. 
  9. "Freight Professionals". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-10-23. Iliwekwa mnamo 2011-12-10. 
  10. "cceia.org". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-09-27. Iliwekwa mnamo 2011-12-10. 
  11. "WikiSummaries".