Dado

(Elekezwa kutoka Audoeni)

Dado (pia: Audoin, Audoen, Owen na Ouen wa Rouen; Sancy, Ufaransa, 609Clichy, Ufaransa, 686)[1][2][3] alikuwa waziri wa Wafaranki na halafu askofu.

Sanamu ya Mt. Audoin (kushoto) na Mt. Waninge (kulia), huko Fécamp, Ufaransa.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 24 Agosti[4].

Maisha hariri

Mtoto wa mtakatifu Authaire (Audecharius), alilelewa katika ikulu ya mfalme Chlothar II (aliyefariki 629), ambapo alipata elimu na uanajeshi pamoja na vijana wengine wa koo maarufu.

Baadaye alisimamia mali ya Dagobert I[5], akishika sana maadili[6] na akiwa na marafiki kama watakatifu Wandregisel, Didier wa Cahors na Eligius, ambaye Dado aliandika habari za maisha yake.

Mwaka 635 pamoja na ndugu zake Ado na Rado alianzisha abasia ya Rebais, halafu monasteri ya Mt. Wandrille huko Rouen, na nyingine ya kike huko Fécamp.

Mwaka 641 alifanywa askofu wa Rouen, jimbo aliloliongoza vizuri kwa miaka 43, akijenga makanisa na monasteri.[5][7]

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. "Reference to the name on Oxford Reference website".
  2. "Example of the use of this spelling". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-05-09. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)
  3. "Example of the use of this spelling".
  4. Martyrologium Romanum
  5. 5.0 5.1 Fouracre, Paul and Gerberding, Richad A., Late Merovingian France, Manchester University Press, 1996 ISBN|9780719047916
  6. The Chronicle of Fredegar, IV, Ch.78, (J.M. Wallace-Hadrill, ed.), London, 1960, p. 66
  7. https://www.santiebeati.it/dettaglio/91517

Vyanzo hariri

  • Alban Butler's Lives of the Saints, edited, revised and supplemented by Thurston and Attwater - Christian classics, Westminster, Maryland.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.