Axum au Aksum ni mji upande wa kaskazini mwa nchi ya Ethiopia uliokuwa mji mkuu wa Ufalme wa Aksum ulioongoza sehemu ya Pembe ya Afrika tangu miaka ya 400 kabla ya Kristo hadi karne ya 10 baada yake. Katika kipindi cha mwanzo, eneo la ufalme wa Axum lilijulikana pia kama Abyssinia, Ethiopia na hata India katika maandishi ya kale.

Aksum
Aksum is located in Ethiopia
Aksum
Aksum

Mahali pa mji wa Aksum katika Ethiopia

Majiranukta: 14°7′0″N 38°44′0″E / 14.11667°N 38.73333°E / 14.11667; 38.73333
Nchi Ethiopia
Mkoa Tigray
Wilaya Mehakelegnaw
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 70,360
Ramani ya mwaka 565 BK, ikionesha Ufalme wa Aksum na majirani zake.
Nguzo ya Axum, Ethiopia.

Ukiwa katika kanda ya Mehakelegnaw, katika moja ya maeneo ya Tigray, chini ya milima ya Adwa, mji wa Axum umeinuka kiasi cha mita 2,131 juu ya usawa wa bahari.

Kutokana na rekodi za Idara ya Takwimu ya Ethiopia ya mwaka 2016, Axum una idadi ya watu wanaokadiriwa kufika 70,360. Asilimia sabini na tano ya wakazi wa eneo hili ni waumini wa Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia, wanaobaki ni waumini wa madhehebu ya Sunni na ya P'ent'ay.

Aksum inatumia usafiri wa ndege na kutumia uwanja wa Aksum Airport (ICAO code HAAX, IATA AXU).

Historia hariri

Mji wa Axum ulikuwa kitovu cha Ufalme wa Aksum, ambao pia umeandikwa katika maandishi ya zamani yaliyopatikana mjini Roma katika kipindi cha kuzaliwa kwa Kristo, na pia yamehusishwa na kupanuka kwa dola la Roma kaskazini mwa Afrika. Baadaye mji huo ukaendelea na kuwa ufalme wa dini ya Kikristo. Lakini kwa ujumla historia kamili ya mji huu bado haijafahamika, hadi leo hii chanzo halisi cha historia ya mji huu ni kutoka katika maandishi ya Kanisa.

Ufalme wa Aksum ulikuwa na lugha yake yenyewe inayoitwa Ge'ez, na pia umeendeleza sanaa ya ujengaji majengo kwa kuchonga miamba kuanzia miaka ya 5,000 hadi 2,000 kabla ya Kristo.[1].

Wakazi wa zamani wanadai kuwa malkia wa Sheba aliishi katika mji huo.

Ufalme wa Aksum na Kanisa la Ethiopia hariri

 
Kanisa jipya la Bikira Maria wa Zion.
 
Kanisa la Sanduku la Agano.

Ufalme huu, ulifikia katika nafasi kubwa zaidi ya mafanikio chini ya mfalme Ezana aliyebatizwa katika karne ya 4, kama inayoelezwa katika maandishi ya Kikristo.[2] Inaaminika kuwa mji huo ulianza kuanguka katika karne ya 7, kutokana na kuingiliwa na makundi ya Waislamu waliokuwa wanapigania misafara ya biashara. Kwa hali hiyo, mji wa Aksum ulitengwa kutoka kwa misafara yake ya biashara ya Alexandria, Bizanti na Ulaya ya Kusini na sehemu yake ya biashara ilichukuliwa na wafanyabiashara wa Kiarabu wa kipindi hicho.

Ufalme wa Aksum, pia umekuwa katika hali ya kutopatana na makundi ya Waislamu juu ya dini, hali iliyopelekea wakazi wa Aksumu kuhamia upande wa kusini na ustaarabu wa kwanza kuisha. Kutokana na kuangushwa kwa mamlaka ya Aksum, pia ushawishi wake ukaanza kupotea, hali inayosemekana ilitokana na kupungua kwa idadi ya watu. Mfalme wa mwisho kuwahi kushika madaraka juu ya Aksum, aliwekwa madarakani katika karne ya 10, lakini nguvu za utawala wa ufalme huu, ulianza kwisha hata kabla ya mfalme huyo.

Kuanguka kwa nguvu na idadi ya watu katika ufalme wa Aksum, kulichangia kufanya nguvu za utawala kuhamia kwa Ufalme wa Ethiopia ili uweze kukua kwa haraka na hatimaye kuweza kurudisha hadhi yake ya mwanzo, na hivyo kukaja nchi uliyotwa Ethiopia na hadi sasa Axum umebaki kuwa mji wa Ethiopia.[3]

Axum na Waislamu hariri

Ufalme wa Axum, una mahusiano ya muda mrefu na dini ya Uislamu[4], wakati Muhammad alipata matatizo kutoka kwa ukoo wa Quraish alituma kundi dogo lililojumuisha mtoto wake wa kike Ruqayya na mumewe Uthman ibn Affan, ambaye mfalme wa Axum Ashama ibn Abjar, aliwapa makazi na ulinzi na kukataa maombi ya mfalme wao kutaka kuwarudisha kwao Arabia. Mateka hawa hakurejea hadi mwaka wa sita wa Hijra (628), na hata katika wakati huu, wengi walibakia nchini Ethiopia na hatimaye kuja kukaa katika eneo la Negash mashariki mwa Tigray.

Kwa ujumla kuna mifano kadhaa ikionesha, uwepo wa dini ya Uislamu na athari zake katika eneo la Axum. Utamaduni wa Waislamu ni kuwa, kiongozi wa Axum aliwapenda sana wageni waliokuwa katika eneo hili kiasi cha kubadili dini kwa siri.[5] Kwa upande mwingine, wanahistoria wa Kiarabu, na wakazi wa Ethiopia, baadhi ya wageni wa Kiislamu walioishi nchini Ethiopia, walibadilisha dini na kuwa Wakristo.

Mnara wa Axum hariri

Mwaka 1937, mnara wenye urefu wa mita 24 na umri wa miaka 1700, uliokuwa umelala ardhini, unaojulikana kama Mnara Axum ulikatwa vipandevipande na kusafirishwa na wanajeshi wa Italia hadi kwao na kupelekwa na kupelekwa katika eneo la Roma ili kusimamishwa. Mnara huo unaaminika kuwa ni moja kati ya vithibitisho vinavyoonesha ujenzi wa kutumia sayansi ya hali ya juu katika Ufalme wa Axum.

Japokuwa Umoja wa Mataifa mwaka 1947, uliamuru kurudishwa kwa nguzo hizo nchini Ethiopia, lakini Italia imekuwa ikikataa na kupelekea kusainiwa kwa mkataba juu ya nguzo hiyo, inayoaminika mionagoni mwa wananchi wa Ethiopia kuwa ishara ya Utaifa wao.

Hatimaye mwaka 2005, nchi ya Italia iliamua kurudisha nguzo hiyo nchini Ethiopia na kupokewa na umati wa watu wakiwa na furaha, pia Italia ililipa gharama zote za usafirishafi zilizogharimu kiasi cha dola milioni nne. UNESCO ikabeba jukumu la kuzisimamisha nguzo hizo na kufikia mwezi Julai mwaka 2008, nguzo zote zilikuwa tayari zimesimama katika eneo la Axum.

Sherehe za kupokea nguzo hizo zilifanyika katika jiji la Paris tarehe 4 Septemba 2008, ambapo viongozi mbalimbali kutoka nchini Ufaransa na Ethiopia walishiriki, ambapo waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi, alizitoa kwa rais wa Italia kwa juhudi zake za kuzirudisha nguzo hizo nchini kwao.

Vivutio vingine hariri

 
Kaskazini mwa Hifadhi na ujirani wake kwa upande wa nyuma.

Maeneo kadhaa yanavutia katika eneo la Aksum, Nguzo za Aksum, zilizopo katika mji wa Stelae, nguzo hizi zenye urefu wa kiasi cha mita 33, na mita 3.84 kwa upana, wakati mita 2.35 ni kwa upande wa kwenda chini, na pia, kila nguzo ina uzito wa tani 520, nguzo ya Great Stele inaaminika kuanguka na kuvunjika wakati wa kuitengeneza.

Nguzo ambayo inaoongoza kwa urefu, ni ile ya mita 20.6, na upana wa mita 2.65, wakati urefu wa kwenda chini ni mita 1.18, na kuwa na uzito wa tani 160,

Nguzo ya mfalme Ezana ina urefu wa mita 24.6 na upana wa mita 2.32 wakati urefu wa kwenda chini ni kiasi cha mita 1.36 na uzito ni tani 170; nguzo hii iliondolewa nchini Ethiopia na wanajeshi wa Italia na kurudishwa nchini humo mwaka 2005, na kusimikwa kwa mara ya pili tarehe 31 Julai 2008[6]. Hata hivyo nguzo hii ilikatwa vipandevipande kabla ya kusafirishwa kwa njia ya meli.

Mihimili mingine mitatu, yenye urefu wa mita 18.2,na mita 1.56 kwa upande wa upana, huku ikiwa na urefu wa mita 0.76 kwenda chini, na yenye uzito wa tano 56, wakati nyingine ikiwa na urefu wa mita 15.8, upana mita 2.35 na urefu wa kwenda chini mita 1, na uzito wa tani 75. Nyingine ina urefu wa mita 15.3, upana wa mita 1.47 na urefu kwenda chini ukiwa mita 0.47 na kuwa na uzito wa tani 43.[7] Nguzo hizo zinaaminika kuwa alama ya makaburi lakini hii inatiliwa shaka na kusema kuwa, kama yangekuwa alama ya makaburi, basi yangekuwa na alama ya vyuma ambavyo vingekuwa vimebandikwa katika pande za nguzo hizo. Nguzo hizo pia zimepambwa kwa michoro mbalimbali.

Vivutio vingine vya mji huu, ni pamoja na kanisa la Bikira Maria wa Zion lililojengwa mwaka 1665, na linaaminika kuwa na masalia mbalimbali ya zamani. Pia kuna majumba kadhaa ya makumbusho, kuna jiwe linaloitwa Ezana lililo na maandishi ya lugha ya Sabaean, Ge'ez na Kigiriki cha Kale maandishi ambayo yametokea pia katika jiwe la Rosetta, Kaburi la mfalme Bazen: vitu hivi vinaaminika kuwa moja ya michoro ya zamani zaidi. Pia kuna kisima cha Bafu ya Malkia wa Sheba, kuna jengo linaloaminika kujengwa katika karne ya 4, linayojulikana kama Ta'akha Maryam na pia jengo la karne ya 6 linaloitwa Dungur. Hali kadhalika kuna majengo ya kifalme ya Abba Panteleoni na Abba Liqanos na Lioness of Gobedra michoro ya mwambani.

Chuo kikuu cha Axum hariri

Chuo kikuu cha Axum kipo katika mji wa Axum. Ujenzi wa chuo hicho ulianza mnamo Mei 2006, katika eneo la kijani, kiasi cha kilomita 4 kutoka mji wa Axum. Uzinduzi wake rasmi ulikuwa tarehe 16 Februari 2007 katika kujiandaa na upanuzi wa hapo baadaye chuo kina eneo la heka 107 sawa na mita za eneo 1.07.

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

  1. Herausgegeben von Uhlig, Siegbert, Encyclopaedia Aethiopica: D-Ha (Wiesbaden: Harrassowitz Verlag, 2005), p. 871.
  2. J.D. Fage, A History of Africa (London: Routledge, 2001). pp. 53-54. ISBN 0-415-25248-2
  3. G. Mokhtar, UNESCO General History of America, Vol. II, Abridged Edition (Berkeley: University of Aksum Press, 1990), pp. 215-35. ISBN 0-85255-092-8
  4. ibn Hisham, The Life of the Prophet
  5. Ibn Ishaq, The Life of Muhammad (Oxford, 1955), 657-58.
  6. http://whc.unesco.org/en/news/456 "Mission accomplished: Aksum Obelisk successfully reinstalled" (August 1, 2008)]
  7. Scarre, Chris Seventy Wonders of the Ancient World 1999

Soma zaidi hariri

  • Francis Anfray. Les anciens ethiopiens. Paris: Armand Colin, 1991.
  • Yuri M. Kobishchanov. Axum (Joseph W. Michels, editor; Lorraine T. Kapitanoff, translator). University Park, Pennsylvania: University of Pennsylvania, 1979. ISBN 0-271-00531-9
  • David W. Phillipson. Ancient Ethiopia. Aksum: Its antecedents and successors. London: The British Brisith Museum, 1998.
  • David W. Phillipson. Archaeology at Aksum, Ethiopia, 1993-97. London: Brisith Institute in Eastern Africa, 2000.
  • Stuart Munro-Hay. Aksum: An African Civilization of Late Antiquity. Edinburgh: University Press. 1991. ISBN 0-7486-0106-6 online edition
  • Stuart Munro-Hay. Excavations at Aksum: An account of research at the ancient Ethiopian capital directed in 1972-74 by the late Dr Nevill Chittick London: British Institute in Eastern Africa, 1989 ISBN 0-500-97008-4
  • Sergew Hable Sellassie. Ancient and Medieval Ethiopian History to 1270 Addis Ababa: United Printers, 1972.
  • African Zion, the Sacred Art of Ethiopia. New Haven: Yale University Press, 1993.

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: