Basmala (Ar. بسملة‎ basmala) ni jina kwa maneno ya Bismillah (بسم الله‎ "Kwa jina la Mungu/Allah", kamili "b-ismi-llāhi r-raḥmāni r-raḥīmi") ambayo ni maneno ya ufunguzi kwa sura za Qurani[1]. Ar-rahman („mwenye rehema“) na Ar-rahim („mwenye neema“) ni pia kati ya majina 99 ya Allah.

Basmala kama kaligrafia kwa maandishi ya Kiarabu.

Waislamu hutumia maneno haya mara nyingi kwa mfano kila wanapoanza sala au kazi muhimu kama vile kabla ya kula chakula, kabla ya safari, wakati wa kuingia katika msikiti, wakati wa kuzika maiti.

Katika sanaa ya Kiislamu basmala hutumiwa mara nyingi kama kaligrafia.

Picha hariri

Marejeo hariri

  1. Kila sura ya Qurani isipokuwa sura ya 9 inaanza kwa maneno "b-ismi-llāhi r-raḥmāni r-raḥīmi" yaani "kwa jina la Mungu mwingi wa ehema mwenye kurehemu"

Viungo vya Nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: