Belt Kubwa

(Elekezwa kutoka Belt Mkubwa)

Belt Kubwa (Kidenmark: Storebælt) ni mlangobahari kati ya visiwa vya Zealand (Sjælland) na Funen (Fyn) nchini Denmark. Pamoja na milangobahari ya Belt Ndogo na Oeresund ni sehemu ya njia ya maji inayounganisha Bahari Baltiki na Bahari ya Kaskazini.

Ramani ya Denmark inayoonyesha milangobahari ya Belt Mkubwa, Belt Ndogo na Oeresund

Jiografia hariri

Belt Kubwa ni mlangobahari kubwa nchini Denmark kwa hiyo ni njia muhimu ya kimataifa kwa meli zote zinazozunguka kati ya nchi za Baltiki na bahari ya dunia. Urefu wa Belt Mkubwa kati ya visiwa vya Zealand an Funen ni kilomita 60 na upana wake ni 16-32 km.

Upande wa kusini inaendelea katika Langelandsbælt bainya ya visiwa vya Langeland na Lolland inayohesabiwa kama sehemu yake.

Belt Kubwa ilipitiwa kwa feri kwa karne nyingi lakini tangu 1997 kuna handaki ya reli chini ya bahari na tangu 1998 daraja la Storebæltsbroen linavukisha belt.

Ekolojia hariri

Kiekolojia Belt Kubwa ni muhimu sana kwa sababu robo 3 za maji yanayobadilishwa kati ya Bahari Baltiki na Bahari ya kaskazini yanapita humo. Bahari ya Baltiki huwa na chumvi kidogo kwa hiyo maji yake ni mepesi kuliko maji ya Bahari ya Kaskazini yenye chumvi zaidi. Hapo maji mazito zaidi kutoka Bahari ya Kaskazini yanaelekea kusini kwenye kina kikubwa juu ya tako la bahari na maji mepesi yenye chumvi kidogo yanaelekea kaskazini juu ya majo mazito zaidi.

Kuna hofu ya kwamba nguzo za daraja zitasababisha kuchanganya kwa tabaka zote mbili na hii ingepunguza kiwango cha oksijeni inayopelekwa Bahari Baltiki maana maji ya Bahari kazskazini huwa na oksijeni zaidi.