Bendera ya Mexiko ina milia mitatu ya wima ya rangi kijani kibichi, nyeupe na nyekundu. Rangi hizi zimetumiwa tangu mapamabano kwa ajili ya uhuru wa Mexiko kutoka Hispania mw. 1821.

Bendera ya Mexiko

Katikati iko nembo la taifa linaloonyesha tai anayekalia mpungate na kushika nyoka.

Upana wa milia na umbo la nembo imewahi kubadilishwa mara nane katika Historia ya Mexiko. Bendera jinsi ilivyo leo ilikubaliwa mwaka 1968 lakini muundo wa milia mitatu na rangi imepatikana tangu 1821.

Rangi zilitajwa mara kwadhaa kuwa na maana. Lakini maelezo haya si rasmi hivyo maelezo yamebadilika mara kadhaa.

Mfano wa elezo ni:

  • Kijani: Tumaini
  • Nyeupe: Umoja
  • Nyekundu: Damu ya washujaa wa uhuru