Benki ya Dunia na Kenya

Benki ya muungano ya nchi ya kenya na benki ya dunia

Benki ya Dunia imetoa msaada wa kifedha kwa miundombinu na mipango ya maendeleo nchini Kenya kuanzia Mei 1960.[1]

Mradi wa kwanza wa Kenya ambao ulifadhiliwa na Benki ya Dunia ulikuwa Mradi wa Kilimo wa Afrika, Benki ya Dunia ilitoa kwa eneo lililokuwa koloni la Uingereza wakati huo dola milioni 5.6 kuwekeza katika miundombinu ambayo ilikuwa muhimu kukuza sekta ya kilimo ya Kenya.[2]

Benki ya Dunia imelinda uhusiano wake na Kenya na inaendelea kufadhili miradi ya maendeleo. Kenya inapokea mikopo kutoka vyombo vya IDA na IBRD kama mawakala wa Benki ya Dunia ambayo imeundwa kusaidia nchi zenye kipato cha chini na cha kati.[1] Benki ya Dunia imeelezea hadharani msaada wake kwa Ajenda ya 4 ya Rais Uhuru Kenyatta, ambayo inakusudia kukuza sekta ya uzalishaji za nchini  Kenya wakati wa kuboresha upatikanaji wa huduma za afya, lishe, na makazi ya bei nafuu.[3] Benki ya Dunia pia imeelezea kuunga mkono "Maono ya mwaka 2030" ya Kenya, ambayo ni mchoro wa maendeleo kugeuza Kenya kuwa taifa la mapato ya kati ifikapo 2030.[4] [5]

Mkurugenzi wa Benki ya Dunia katika nchi ya Kenya ni C. Felipe Jaramillo, pia anafanya kama mkurugenzi wa nchi ya Rwanda, Somalia, na Uganda.[6] [7] Benki ya Dunia imeongeza thamani ya kukopesha kwake Kenya katika miaka ya hivi karibuni, kutoka $ 623 milioni mwaka 2019 hadi $ 1.27 bilioni mwaka 2019.[8]

Marejeo hariri

  1. 1.0 1.1 "Projects". World Bank (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-08-19. 
  2. "Development Projects : African Agriculture Project - P001218". World Bank (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-08-19. 
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-12-03. Iliwekwa mnamo 2021-08-23. 
  4. https://www.worldbank.org/en/programs/sdgs-2030-agenda
  5. https://vision2030.go.ke/
  6. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-12-03. Iliwekwa mnamo 2021-08-23. 
  7. "Carlos Felipe Jaramillo". World Bank (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-08-23. 
  8. "Economic Memorandum: Kenya’s Growth Story: Past, Present and Future". World Bank (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-08-23.