Bernadi wa Parma (Firenze, Italia, 1060 hivi – Parma, Italia, 4 Desemba 1133) alikuwa mmonaki na mkuu wa urekebisho wa Wabenedikto wakaapweke wa Vallombrosa.

Mt. Bernadi alivyochorwa na Pietro Perugino.

Alifanywa kardinali na askofu wa Parma kuanzia mwaka 1106 hadi kifo chake.

Tangu wakati huo aliheshimiwa kama mtakatifu. Mwaka 1139 Papa Inosenti II alipitisha sifa hiyo[1] [2].

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 4 Desemba[3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Salvador Miranda. "Uberti, O.S.B.Vall., Bernardo degli (ca. 1060-1133)". The Cardinals of the Holy Roman Church. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-06-09. Iliwekwa mnamo 27 September 2017.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. http://www.santiebeati.it/dettaglio/80450
  3. Martyrologium Romanum

Vyanzo hariri

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: