Bice Osei Kuffour

Mwanamuziki na Mjasiriamali wa kijamii

Bice Osei Kuffour (alizaliwa 17 Novemba ,1981) ni mwanamuziki wa hiplife wa nchini Ghana, anayejulikana kwa jina la Obour, ambalo linamaanisha "jiwe" katika lugha ya Kiakan . Alikua Rais wa Muungano wa Wanamuziki wa Ghana, [1] katika kundi la umbrella group ambalo linaunganisha wanamuziki wote nchini Ghana bila kujali aina ya muziki. [2] Bice Osei Kuffour alishiriki uchaguzi wa mchujo wa NPP katika eneo la bunge la Asante Akyem Kusini kama mgombea ubunge. Baadae aliteuliwa kuwa katibu wa kamati ya Matangazo ya kampeni ya NPP 2020. Obour ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Ghana, Ni mwanaharakati wa kijamii ambaye ni balozi wa kitaifa wa usalama barabarani; Balozi wa WHO wa Kifua Kikuu Baraza la Uingereza & Tume ya Misitu ya Ghana na Balozi wa Mabadiliko ya Tabianchi. Pia ni rais na Mwanzilishi wa shirika la Christiana Addo Memorial Foundation ambalo linakuza elimu, usafi wa mazingira, usafi wa kibinafsi na uwezeshaji wa vijana huko Asante Akyem.[3]

Bice Osei Kuffour
Rais wa Muungano wa Wanamuziki wa Ghana - MUSIGA, Bice Osei Kuffour akizungumza kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Creative Commons 2011 huko Warsaw, Poland.
Rais wa Muungano wa Wanamuziki wa Ghana - MUSIGA, Bice Osei Kuffour akizungumza kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Creative Commons 2011 huko Warsaw, Poland.
Alizaliwa 17 Novemba 1981
Nchi Ghana
Kazi yake Mwanamuziki

Maisha na kazi hariri

Obour alizaliwa "Braha Bebu Me" (Dekyemenso) katika Mkoa wa Ashanti mnamo 7 Novemba 1981, na Christiana Addo na Mchungaji BO Kuffour. Akiwa na umri wa miaka sita, Obour alicheza ngoma za aina nyingi, hasa Atumpan, katika jumba la chifu la Juaso-Ashanti Akyem ambako baba yake alikuwa akiongoza. Obour alisoma katika mbalimbali kama Shule ya Majaribio ya Jimbo ( Kumasi ), Shule ya Kliniki ya Soul ( Accra ), Shule ya Sekondari ya Garison Junior ( Kambi ya Burma ) na Shule ya Mfantsipim ( Cape Coast ).

Baada ya kumaliza shule ya upili, Obour aliomba usaidizi kutoka kwa binamu yake aliyeishi London, J. Amano, ambaye alimuunganisha na lebo yake ya binafsi ya Soul Records. Baadae alitoa wimbo wa Atentenben ambao ulishinda tuzo tatu za Soul Records kwenye tuzo za muziki za Ghana (Ghana Music Awards) mnamo 2002, pamoja na Video ya mwaka. Nyimbo hizi, na zingine za lebo hiyo, zilipelekea Soul Records kutunukiwa kama Record Lebo bora ya Mwaka. Video hiyohiyo ilishinda tuzo bora zaidi katika tuzo za muziki za Our Music Awards (OMA) mnamo 2002.

Marejeo hariri

  1. "Obour Elected MUSIGA President". www.modernghana.com. Iliwekwa mnamo 19 August 2011.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. Selase Attah, "Pressure mounts on Obour as MUSIGA elections loom" Archived 24 Julai 2015 at the Wayback Machine., Ghanaie.com, 12 June 2015.
  3. https://mobile.ghanaweb.com/person/Bice-Osei-Kuffour-338
  Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bice Osei Kuffour kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.