Bobby Farrell (6 Oktoba 1949 mjini Aruba - 30 Desemba 2010) alikuwa mwimbaji wa kiume wa bendi ya muziki wa pop na disco-Boney M., kunako miaka ya 1970.

Bobby Farrell
Hii picha ya kundi la muziki la Boney M. Kutoka kushto kuelekea kulia; Liz Mitchell, Bobby Farrell, Maizie Williams, na Marcia Barrett.
Hii picha ya kundi la muziki la Boney M.
Kutoka kushto kuelekea kulia;
Liz Mitchell, Bobby Farrell, Maizie Williams, na Marcia Barrett.
Maelezo ya awali
Amezaliwa (1949-10-06)Oktoba 6, 1949
Asili yake Aruba
Amekufa 30 Desemba 2010 (umri 61)
St. Petersburg, Urusi
Aina ya muziki Pop, Disco
Kazi yake Dancer, mburudishaji
Miaka ya kazi 1975–hadi leo
Studio Hansa Records, Sony-BMG

Farrell aliondoka mjini Aruba akiwa na umri wa miaka 15 na baada ya hapo akaja kuwa baharia. Farrel pia aliwahi kuishi nchini Norway na Uholanzi kabla ya kuhamia nchini Ujerumani. Akiwa huko, alifanya kazi nyingi akiwa kama Dj na baadaye akakutana na mtayarishaji wa muziki wa Kijerumani bwana Frank Farian na akamtaka Farrell awe mmoja wa wanakundi lake la muziki maarufu kama Boney M. Farrell akaja kuwa mwimbaji pekee wa kiume katika bendi hiyo, ingawaje, Farian baadaye alisema kwamba Bobby hakufanya kazi sehemu kubwa sana, na akasema kwa kila wanapo ingiza sauti katika nyimbo basi nayeye Farian hushriki katika rekodi hizo. Farrell alikuwa akifanya hadi matamasha ya maukumbi mbalimbali.

Kunakko mwaka wa 2005 Farrell alionekana kama mchezaji katika sehmu ndogo ya video ya mwanamuziki Roger Sanchez, nyimbo ilikuwa Turn on the Music.

Farrell kwa sasa hivi anaishi mjini Amsterdam.

Albamu alizotoa hariri

Nyimbo maarufu

  • 1982: Polizei / A Fool In Love
  • 1985: King OF Dancing / I See You
  • 1987: Hoppa Hoppa / Hoppa Hoppa (Instrumental)
  • 1989: Tribute To Josephine Baker
  • 2004: Aruban Style (Mixes) S-Cream Featuring Bobby Farrell
  • 2006: The Bump EP

Bobby Farrell na Boney M. / Boney M. Wakishrikiana na Bobby Farrell / Bobby Farrell Akishirkiana na Sandy Chambers

  • 2000: The Best Of Boney M. (DVMore)
  • 2001: Boney M. - I Successi (DVMore)
  • 2001: The Best Of Boney M. (II) (compilation)
  • 2001: The Best Of Boney M. (III) (compilation)
  • 2005: Boney M. - Remix 2005 (featuring Sandy Chambers) (nyimbo mchanganyiko) (Crisler)
  • 2007: Boney M. - Disco Collection (compilation)

Tafadhali elewa kwamba: Matoleo yote ya yaliyoingiliana na rekodi za vibao vya Boney M.- basi elewa kwamba havikuwa katika matoleo halisi ya albamu za Boney M.

Vingo vya Nje hariri