Bunge la jimbo la Illinois

(Elekezwa kutoka Bunge la jimbo la Illinos)

Bunge la juu la jimbo la Illinois, nchini Marekani, ni baraza kuu katika dola hili likiwa na jukumu la kupitisha sheria zinazohusu jimbo hilo. Bunge hilo lilibuniwa kupitia katiba ya jimbo, iliyopitishwa mwaka 1818. Lina wabunge 59 wanaochaguliwa kila mmoja kutoka sehemu wakilishi bungeni, wale wabunge wakigawiwa katika makundi matatu, na kila kundi likipigiwa kura tena baada ya muhula wa miaka miwili.[1]

Bunge hili huketi katika mji wa Springfield, Illinois. Barack Obama alikuwa mjumbe katika bunge hili kwa mihula mitatu, kabla ya kuchaguliwa kujiunga na Bunge La Maseneta La Marekani mwaka 2004.

Marejeo hariri

  1. Katiba ya Illinois Kipengele cha Nne, Aya 2(b) http://www.ilga.gov/commission/lrb/con4.htm

Viungo vya Nje hariri