Bustani za Botanic

Bustani za Botanic Belize (kwa Kiingereza: "Belize Botanic Gardens", kifupi: BBG) ni hekari 45 zenye mimea ya asili na ya kigeni inayokua katika wilaya ya Cayo ya Belize magharibi.

Mmoja wa mimea katika bustani.

Bustani ipo katika bonde la Mto Macal, iliyozungukwa na mlima wa Maya.

Lengo kuu la BBG ni kuhimiza kilimo endelevu, kudumisha makusanyo ya hifadhi na kushiriki katika elimu ya uhifadhi. Inalenga kuhamasisha wageni ili kulinda mimea na makazi yao kwa kujifunza zaidi kuhusu ulimwengu wa mimea.