Bwawa la Malebo (far. Pool Malebo, majina mengine Malebo Pool, zamani Stanley Pool, pia Ziwa Ngobila au Ziwa Nkunda) ni sehemu ya mwendo wa mto Kongo ambako mto unapanuka sana kwa urefu wa kilomita 35 ukifikia upana wa kilomita 23.

Bwawa la Malebo linavyoonekana kutoka chombo cha angani (picha ya NASA)
Bwawa la Malebo linavyoonekana kwa macho ya ndege kutoka upande wa Kinshasa


Jina hariri

Jina la Malebo latokana na jina la kienyeji "lilebo (uwingi malebo)" kwa miti ya aina mchapa[1] (Borassus flabellifer) inayopatikana kwa wingi hapo.

Jina la zamani Stanley Pool latokana na Henry Morton Stanley aliyefika hapa mwaka 1877 akaanzisha kituo cha Léopoldville , kitangulizi cha mji wa Kinshasa.

Jiografia hariri

Miji mikuu ya Kinshasa na Brazzaville iko kando la bwawa hili ikitazamana.

Sehemu ya mto Kongo inayopitika kwa meli ndogo za mtoni kwenda hadi Mbandaka, Kisangani na Bangui inaanza hapa. Chini ya bwawa kuna maporomoko ya Livingstone[2] yanayozuia usafiri kwa maji hadi bahari.

Marejeo hariri

  1. Majina ya Kiswahili ni mchapa, mtappa au mvomo / mvumo, ling. [1]
  2. Stanley, H.M., 1899, Through the Dark Continent, London: G. Newnes, Vol. One ISBN 0486256677, Vol. Two ISBN 0486256685

Viungo vya Nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: