Cape Town Tigers ni klabu ya mpira wa kikapu nchini Afrika Kusini yenye makao yake jijini Cape Town.[1] Timu hiyo inapatikana katika kitongoji cha Gugulethu.[2] Ilianzishwa mwaka 2019, makocha ni Raphael Edwards na Vincent Ntunja. Mwaka 2021, klabu ilishinda ubingwa wa kitaifa Afrika Kusini ukiwa msimu wake wa kwanza katika mashindano hayo.

Mataji hariri

Michuano ya kitaifa Afrika Kusini

  • Mabingwa (2): 2021, 2022

Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika

  • Mshindi wa Robo fainali[3] (1): 2022

Marejeo hariri

  1. "We Are The Tigers". www.capetowntigers.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-09-02. 
  2. "Cape Town Tigers", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2022-08-23, iliwekwa mnamo 2022-09-02 
  3. "Cape Town Tigers at the ROAD TO BAL 2022 2021". FIBA.basketball (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-09-02.