Charles Beh ni mfanyabiashara wa nchini Liberia. Ni mmiliki wa kituo cha Biashara cha Charles Business Center (CBC), na duka maarufu la rejareja katika mtaa wa Randall Street katikati mwa mji wa Monrovia.

Beh alianza kuuza jeans na nguo za michezo mnamo 1993 wakati wa vita ya kwanza ya wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia.

Mnamo 2001, alijiunga na Benki ya Liberia ya Maendeleo na Uwekezaji kwa mkopo wa dola za kimarekani 50,000 kutoka kwenye mpango wa mkopo kwa vijana wajasiriamali (YEP). Leo anaendesha maduka mawili ya bidhaa za jumla za nguo viatu na mikoba ya wanawake katika mtaa wa Water Street.[1]

Marejeo

hariri
  1. "Businessman Raps on Doing Business, Finding Financing". Liberian Observer. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 13 Julai 2012. Iliwekwa mnamo 28 Aprili 2012.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Charles Beh kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.