Chuo Kikuu cha Benin

Chuo Kikuu cha Benin kilichopo katika jiji la Benin, jimbo la Edo, ni moja ya vyuo vikuu vilivyo vikubwa zaidi nchini Nigeria.

Chuo Kikuu cha Benin
Chuo Kikuu cha Benin
Wanafunzi40,000
MahaliBenin City, Nigeria
6°40′N 6°0′E / 6.667°N 6.000°E / 6.667; 6.000Coordinates: 6°40′N 6°0′E / 6.667°N 6.000°E / 6.667; 6.000
Tovutiwww.uniben.edu

Hufundisha masomo mbalimbali, yakiwa pamoja na utabibu. Ina wanafunzi takriban 36,000.

Historia hariri

Chuo kikuu kilianzishwa mwaka 1970 na serikali ya kijeshi ya Samuel Ogbemudia.[1]

Kilianza kama Taasisi ya Teknolojia na kilipewa hadhi ya Chuo Kikuu na Tume ya Taifa ya Vyuo Vikuu (NUC) tarehe 1 Julai 1971. Katika hotuba yake ya Bajeti mnamo Aprili 1972, aliyekuwa Gavana wa jeshi la jimbo la magharibi ya kati, Kanali S.O. Ogbemudia alitangaza mabadiliko ya jina la Taasisi ya Teknolojia ya Chuo Kikuu cha Benin.

Katika mwanzo, chuo kikuu kilikuwa katika barabara ya Ekewan. Mwaka 1972, mradi wa kujenga kampasi kuu katika Ugbowo na Ekosodin ulianzia na Mhandisi Daniel Uhimwen kama mkurugenzi. Leo, tovuti kuu iko Ugbowo lakini bado baadhi ya kozi zinazotolewa katika kampasi ya Ekewan.

Tarehe 1 Aprili 1975, katika Chuo Kikuu,kufuatilia pendekezo la Jimbo la Serikali, kilichukuliwa juu na Serikali na kikawa Chuo Kikuu cha Jimbo. Leo, Chuo Kikuu kimeendelea kukua katika nguvu kwa idadi ya Vitivo, Idara, Mashirika na Kozi.

Mwaka 1985, Grace Alele-Williams akawa makamu wa kike wa kwanza wa Nigeria wakati alipoteuliwa kuongoza Chuo Kikuu cha Benin. Yeye akatumikia kama Makamu wa Chansela hadi 1991.

Vitivo na kozi hariri

Kufuatia maelekezo ya NUC, Chuo Kikuu kilifanya majaribio na mfumo wa vyuo mwaka 1991/92 na 1992/93. Hata hivyo, licha ya maendeleo haya mapya, Chuo Kikuu kilirudi kwa Mfumo wa Vitivo Januari 1994. Sasa; Chuo Kikuu kimsingi hufuata mfumo wa Kitivo System isipokuwa Shule za Utabibu, Utabibu wa Meno, Sayansi, na Taasisi ya Afya ya Mtoto, ambayo ilirudi kwa mfumo wa vyuo mwezi Agosti 1999, na utawala wake ukiwa ni Provosti. Vitivo vilivyoko sasa ni vile vya Kilimo, Sanaa, Elimu, Uhandisi, Sheria, Madawa, Sayansi, Usimamizi na Chuo cha Sayansi ya Utabibu.

Chuo Kikuu hutoa kozi za ngazi mbalimbali: Uzamili, Shahada, Stashahada na Cheti. Hivi sasa, jumla ya wanafunzi waliojisajili na chuo ni 40,000 linaloundwa na wanafunzi wa mchana na jioni katika Vitivo mbalimbali.

Maktaba hariri

Maktaba kuu ya Chuo Kikuu, iitwayo maktaba ya John Harris, ilipewa jina hilo baada ya mwanzilishi, Prof John Harris, kutoka New Zealand. Maktaba kimekuwepo Chuo Kikuu kilipoanza mwaka 1970 katika Barabara ya kampasi ya Ekehuan maktaba ya John Harris is jengo la kisasa yenye fani za hewa. Jengo limebuniwa kuwaketisha wasomaji 700. Huwa na huduma za kutoa nakala, na kufunga vitabu kwa wasomaji. Maktaba sasa inatumia mfumo wa tarakilishi. Ufungaji wa teknolojia ya kisasa nyingine unaendelea. Pamoja na ongezeko la idadi ya wanafunzi, maktaba imejiingiza katika mpango wa upanuzi wa maktaba ukianza na ujenzi wa maktaba katika vitivo tofauti kama vile maktaba ya barabara ya kampasi ya Ekehuan, Maktaba ya Utabibu, Sheria, Uhandisi na Madawa yote yanafanya kazi. Upanuzi wa maktaba ya John Harris bado inasubiri ruhusa rasmi. Maktaba hushiriki katika ushirikiano kati ya maktaba zingine nchini Nigeria.

Picha hariri

Marejeo hariri

  1. Osamede Osunde. Dr Osaigbovo Ogbemudia. Edo World. Iliwekwa mnamo 2009-11-27.

Viungo vya nje hariri