Alfabeti ya Kilatini
(kwa matumizi ya Kiswahili)
Aa Bb Cc ch Dd
Ee Ff Gg Hh Ii Jj
Kk Ll Mm Nn Oo Pp
Qq Rr Ss Tt Uu Vv
Ww Xx Yy Zz

D ni herufi ya 4 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Delta ya alfabeti ya Kigiriki.

Maana za D hariri

Historia ya D hariri

Hieroglifu ya Misri
mlango
Kisemiti asilia
Mlango (wa hema)
Kifinisia
Dalet
Kigiriki
Delta
Kietruski
D
Kilatini
D
O31
         

Asili ya herufi D ni miandiko iliyotangulia alfabeti ya Kilatini. Waroma walipokea mwandiko kutoka alfabeti ya Kigiriki kupitia alfabeti za Kiitalia za awali kama Kietruski. Wagiriki walipokea kutoka Wafinisia.

Wafinisia walikuwa na alama ya "dalet" iliyokuwa kiasili picha iliyorahisishwa ya mlango wakitumia alama tu kwa sauti ya "d" na kuiita kwa neno lao kwa mlango "dalet". Wagiriki walichukua alama hiyo na kuiita "Delta" bila kujali maana asilia ya "mlango" ilikuwa sauti tu ya "d".

Waitalia wa kale kama Waetruski wakapokea herufi kwa umbo lisilokuwa na kona kali. Waroma wakaichukua lakini waligeuza mwelekeo wake kuwa D jinsi ilivyo hadi sasa.