Daraja la Mfereji wa Suez

Daraja la Suez pia huitwa Suez Canal Bridge, au Shohada 25 Januari Bridge au Egyptian-Japanese Friendship Bridge, ni daraja la barabara linalovuka Mfereji wa Suez (Suez Canal) katika eneo la El Qantara. Neno la kiarabu la "al qantara" linamaanisha "daraja".

Daraja la kuvuka Mfereji wa Suez

Kubuniwa na kujengwa hariri

Daraja hili, lilijengwa kwa msaada wa serikali ya Japan huku Mhandisi akiwa Kampuni ya PentaOcean Construction.

Serikali ya Japan ilitoa kiasi cha asilimia 60 ya gharama za ujenzi hii ikiwa ni kiasi cha Yen bilioni 13.5, hii ilikubaliwa wakati Raisi Mubarak alipoitembelea Japan mwezi Machi mwaka 1995, kama sehemu ya kuendeleza mkono nchi wa Sinai. Misri nayo ilichangia kiasi cha asilimia 40 yaani Yen bilioni 9, zilizobaki. Na daraja likafunguliwa mwezi Oktoba mwaka 2001.

Daraja hili lina nguzo ndefu zinazozishikia zenye muundo wa Nguzo za Farao. Pia daraja hili lina kiasi cha urefu wa mita 68.[1] juu ya mstari wa maji. Au (Suezmax) juu ya meli zinazoweza kupita katika Mfreji huo.

Maendeleo katika eneo la daraja hariri

Daraja la Suez ni moja kati ya njia muhimu za kuleta maendeleo katika eneo la Mfereji wa Suez lakini pia na maeneo ya jirani kama vilee Ahmed Hamdi Tunnel iliyopo katika Mfereji wa Suez, iliyomalizika mwaka 1981 na El Ferdan daraja la reli.

Marejeo= hariri

  1. Art. 52 Rules of Navigation in http://www.suezcanal.gov.eg/

Viungo vya Nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: