Domobuluu
Domobuluu kichwa-chekundu Spermophaga ruficapilla
Domobuluu kichwa-chekundu
Spermophaga ruficapilla
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Passeroidea (Ndege kama shomoro)
Familia: Estrildidae (Ndege walio na mnasaba na mishigi)
Jenasi: Spermophaga
Swainson, 1837
Ngazi za chini

Spishi 3:

Madomobuluu (kutoka Kiing.: bluebill) ni ndege wadogo wa jenasi Spermophaga katika familia Estrildidae ambao wanatokea Afrika tu. Ndege hawa ni baina ya wakubwa kabisa wa familia hii na wana domo fupi na nene sana. Wanafanana na wabanjambegu lakini domo lao ni buluu lenye ncha nyekundu. Kidari ni chekundu, mabawa na mkia ni nyeusi au kahawia na tumbo ni jeusi au kahawia lenye madoa meupe. Hula mbegu hasa na wadudu pia, hususa makinda. Tago lao ni tufe la manyasi, nyuzinyuzi na vigoga lenye mwingilio kwa kando. Jike huyataga mayai 3-4.

Spishi hariri

Picha hariri

  Makala hii kuhusu "Domobuluu" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili bluebill kutoka lugha ya Kiingereza. Neno (au maneno) la jaribio ni domobuluu.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.