East African Breweries

East African Breweries ni kampuni kubwa ya Afrika Mashariki inayotengeneza pombe ambayo inamiliki 80% ya Kenya Breweries, 98.2% ya Uganda Breweries, 100% ya Central Glass -kampuni yakutengeneza glasi, 100% ya Kenya Maltings na 46% ya United Distillers and Vintners (Kenya) Limited, 100% ya Universal Distilers Uganda, 100% EABL International (inayowajibika kwa mauzo ya nje), 100% ya East African Maltings, 100% EABL Foundation na 20% ya Tanzania Breweries.

East African Breweries
Makao MakuuNairobi, KenyaKenya
Owner(s)Jeremiah G. Kiereini(chairman)

Historia hariri

Kenya Breweries ilianzishwa mwaka wa 1922 na walowezi wawili, George na Charles Hurst. Kufikia mwaka wa 1990, wengi wa wanahisa walikuwa kwenye kampuni hii walikuwa Wakenya na ilikuwa na mafanikio sana.

Tanzania Breweries ilikuwa imeanzishwa na Kenya Breweries katika miaka ya 1930. Baada ya kutaifishwa mwaka wa 1967, Tanzania Breweries ilikumbwa na usimamizi mbaya. Hata hivyo, mwaka wa 1993 serikali ya Tanzania aliingia mkataba na South African Breweries Limited kuendesha shughuli za Tanzania Breweries. South African Breweries ni mojawapo wa makampuni makubwa ya kutengeneza pombe na yenye ufanisi mkubwa duniani. Waliimarisha Tanzania Breweries kwa kasi ya ajabu, huku uzalishaji ukiongezeka kwa karibu mara tatu kwa kipindi cha miaka mitatu.

Mwaka wa 2002 East African Breweries Limited (EABL) na SABMiller Plc. walikubaliana kubadilishana hisa zao kwenye kumpuni walizomiliki: Kenya Breweries Limited na Tanzania Breweries Limited. EABL ilipewa 20% ya hisa za Tanzania Breweries. SABMiller Plc. nayo ilipewa 20% ya umiliki kwenye Kenya Breweries. Mnamo mwaka wa 2003, Kenya Breweries ilitumia karibu 6% ya maji ya Nairobi.

Umiliki na Uorodheshaji hariri

Mmiliki mkuu ni Diageo Plc. Uorodheshaji wa msingi wa EABL ni kwenya Soko la Hisa la Nairobi, na pia imeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Uganda na Soko la Hisa la Dar-es-Salaam.

Bidhaa hariri

 
Chupa ya bia ya Tusker.

Tusker ndio brandi kuu ya East African Breweries na zaidi ya 30% ya soko la Kenya la bia huuza zaidi ya hektolita 700,000 kila mwaka. Tusker pia ndio brandi ya bia kuu katika kundi la makampuni la Diageo .[1] Ina kiwango cha pombe cha 4.2% abv. Brandi hii ilianzwa kuuzwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1923, muda mfupi baada ya mwanzilishi wa Kenya Breweries Ltd, George Hurst, aliuawa na ndovu kwenye ajali ya uwindaji. Ilikuwa mwaka huu ambapo alama ya ndovu, inayotambulisha Tusker Lager, ilikubalika. Kaulimbiu "Bia Yangu, Nchi Yangu", maana yake "My Beer, My Country" katika Kiswahili.

Mapema ya mwaka wa 2008, maduka ya supamaketi ya Uingereza ya Tesco yalianza kuuza Tusker, ikifuatiwa baadaye na Sainsbury's [2].

Kampuni hii pia hutengeneza Uganda Waragi , kileo kilicho na kiwango cha pombe cha 40% abv na ni miongoni mwa brandi ya waragi na ndicho kinyuaji kilichonereshwa kinachoongoza kule Uganda. Hutengenezwa kutoka kwa mtama,hunereshwa mara tatu. Kinajulikana nchini Uganda kama "The Spirit of Uganda," au kwa kifupi UG. Masoko makuu ni pamoja na nchi nyingine za Afrika kama vile Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Sudan.[3]

Mnamo mwaka wa 1965, "Sheria ya Bunge ya Enguli" iliamuru kwamba kunereka kungehalalishwa tu chini ya leseni, na waneraji wangepaswa kuuzia kampuni iliyoendeshwa na serikali ya Uganda Distilleries Ltd - iliyozalisha bidhaa kwenye chupa na kuuzwa chini ya jina, Uganda Waragi.

EABL Foundation hariri

EABL Foundation ndio kiungo cha Wajibu kwa jamii cha East African Breweries, ilianzishwa mwaka 2005. Husaidia watu nchini Kenya, Uganda na Tanzania kupitia kwa shuguli za miradi tano: maji, elimu na mafunzo, afya, mazingira, na miradi maalum.

Miradi zake zinazoendelea ni pamoja na ujenzi wa kituo cha macho mjini Moshi; msaada kwa Sickle Cell Association of Uganda; na mchango wa Ultra Sound Machine kwa Kirwara Hospital. Mpango huu umetolea zaidi ya shilingi milioni 70 pesa ya Kenya (takriban $ 972,000) kwa misaada kwa wanafunzxi wa vyuo vikuu.

EABL Foundation hujihusisha na miradi maalum katika nyakati za maafa na kutoa misaada ya dharura wakati inahitajika. Hivi karibuni, ilijiusisha katika Save A Life Fund, ambapo ilichangia zaidi ya Shilingi za Kenya milioni 14 (takribani $ 194,000) kwa kuwasaidia waathiriwa wa njaa.[4]

Tusker FC hariri

Makala kuu: Tusker F.C.

Tusker FC ni kilabu cha kandanda kinachomilikiwa na East African Breweries. Makao yake ni mjini Nairobi, Kenya. Ndicho kilabu cha tatu chenye mafanikio nchini Kenya kikiwa kimeshinda ligi ya Kenya mara nane na kushinda kikombe cha Kenya Cup mara tatu. Aidha, kimeshinda mara nne kombe la Afrika Mashariki la CECAFA Clubs Cup.

Kilabu kilikuwa kinajulikana kama "Kenya Breweries" hadi mwaka wa 1999 wakati kilibadilisha jina hadi la sasa. Tusker FC uwanja mbili wa kuchezea wa nyumbani, Moi International Sports Centre na Ruaraka Sports Ground.

Marejeo hariri

Vidokezo hariri

  1. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-07-22. Iliwekwa mnamo 2021-01-16.
  2. Tusker Lager wins Sainsbury's listing - Talking Retail. Jalada kutoka ya awali juu ya 2008-07-05. Iliwekwa mnamo 2009-12-21.
  3. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2007-03-11. Iliwekwa mnamo 2021-01-16.
  4. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-04-10. Iliwekwa mnamo 2009-12-21.

Makala hariri

  • Justin Willis, Potent Brews: A Social History of Alcohol in East Africa, 1850-1999, British Institute in Eastern Africa (2002), ISBN 082141475

Viungo vya nje hariri