Edina Alves Batista

Edina Alves Batista (alizaliwa 10 Januari 1980) ni mwamuzi wa mpira wa miguu wa chama cha soka cha Brazil. [1]

Kazi hariri

Alikuwa mwamuzi katika michezo miwili mnamo Aprili 2018 kwenye michuano ya kombe la Copa Amerika la Wanawake 2018 iliyofanyika Chile.

Aliongoza mechi kadhaa kwenye Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake 2019 pamoja na nusu fainali kati ya Uingereza na Marekani . [2]

Mwaka 2020, alikuwa mwamuzi katika mashindano ya Kandanda ya Wanawake ya Amerika Kusini 2020 yaliyofanyika nchini Argentina.

Mnamo 7 Februari 2021, alikua mwanamke wa kwanza kuchezesha katika mashindano ya FIFA ya mpira wa miguu wa wanaume, ambapo alichezesha mechi ya nafasi ya tano kati ya Ulsan Hyundai na Al-Duhail kwenye Kombe la Dunia la Vilabu la FIFA la 2020 . [3] Mnamo 3 Machi 2021, alikua mwamuzi wa kwanza wa mwanamke kuchezesha mchezo wa dabi kati ya Corinthians na Palmeiras nchini Brazil. [4]

Marejeo hariri

  1. "Edina Alves Batista agora é FIFA, a notícia foi oficializada pela Confederação Brasileira de Futebol" (kwa Kireno). goioere.cidadeportal.com.br. 16 December 2015. Iliwekwa mnamo 2 July 2019.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  2. "FIFA Women's World Cup France 2019 - List of match officials". 
  3. @FIFAcom (7 February 2021). "History made at the #ClubWC" (Tweet) – kutoka Twitter.  Check date values in: |date= (help)
  4. "O dérbi resiste a tudo e consagra Edina Alves Batista". uol.com (kwa Portuguese). 3 March 2021.  Check date values in: |date= (help)
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Edina Alves Batista kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.