Ni mtanzania mfanya biashara katika sekta ya mazao ya kilimo anaye fahamika kwa kuanzika kampuni ya East Africa Fruits ambayo ni moja ya makampuni makubwa nchini Tanzania. Kampuni hii inajihusisha na kuuza matunda ndani na nje ya Tanzania huku lengo likiwa ni kuongeza thamani kwa mkulima ambaye ameyalima mazao hayo ili aweze kunufaika na kuwa na maisha bora.[1]

Maisha ya Awali na Elimu

hariri

Elia alisoma katika chuo kikuu cha Mzumbe kilichopo Mkoani Morogoro. Kabla ya kuanzisha East Africa Fruits, Elia alishiriki kikamilifu katika kumsaidia mama yake mzazi kwenye biashara zake za kuuza vyakula ambapo pasipo kuwa na elimu kubwa mama yake Eliya aliweza kumiliki migahawa mitano huko mkoani Kilimanjaro. Akiwa anafanya mafunzo kwa vitendo chini ya wizara ya Kilimo, Elia aliweza kuona fursa nyingi ndani ya sekta ya kilimo huku akidhamiria kusaidia kuongeza thamani katika sekta hiyo, ndipo alipo anzisha kampuni yake ya East Africa Fruits[2].

Akiwa Chuoni aliweza fanya Mafunzo kwa vitendo katika wizara ya kilimo. Pia mara baada ya kumaliza chuo alishirikiana na wenzake kuanzisha kampuni iliyo itwa AMEJ investment akiwa kama mkurugenzi na mwana hisa mdogo. Zaidi ni kuwa mwanzilishi na mkurugenzi mkuu wa Kampuni yake ya East Africa Fruits[3].

Tuzo na Teuzi

hariri
  1. African Entrepreneurship Awards (AEA) - 2015
  2. Tuzo ya ABH (Mshindi wa Jumla) - 2022[4]

Marejeo

hariri
  1. "Shortening the long road between farmer and consumer: The East Africa Fruits case". eastafrica.rikolto.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-05-10.
  2. https://fincaventures.com/meet-the-entrepreneur-elia-timotheo-east-africa-fruits/
  3. https://www.crunchbase.com/person/elia-timotheo
  4. "You are being redirected..." panafricanvisions.com. Iliwekwa mnamo 2024-05-10.