Embakasi ni mtaa wa Nairobi, mji mkuu wa Kenya. Uko mashariki mwa katikati ya jiji. Ni mtaa wa makazi na wengi wa raia wanaoishi humo ni wa mapato ya daraja la pili la wastani. Ni kata ya eneo bunge la Embakasi Mashariki, kaunti ya Nairobi.

Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, uwanja wa ndege mkuu Nairobi uko Embakasi na ulijulikana kama Embakasi Airport wakati ulipofunguliwa mwaka wa 1958.

Tarafa ya Embakasi hariri

Embakasi pia ni jina la utawala la tarafa mjini Nairobi. Imegawanywa katika maeneo yafuatayo (sensa ya 1999)[1]

Tukio hariri

Katika masaa ya asubuhi ya 27 Januari 2008, Mbunge wa Eneo Bunge la Embakasi, Mugabe Were alipigwa risasi na washambulizi wawili na kufa. Kulingana na taarifa za habari, Mugabe alikuwa tu amewasili katika boma yake wakati aliposhambuliwa akiwa bado katika gari lake, kabla ya lango kufunguliwa. Mugabe alichaguliwa kuwa mjumbe wa Orange Democratic Movement, chama cha upinzani nchini Kenya. Uvumi kuhusu uwezekano wa mauaji haya kuwa ya kisiasa bado unazingira kifo hiki katika mgogoro uliotokea kuhusu uchaguzi wa rais wa tarehe 27 Desemba 2007[2][3].

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

Coordinates: 1°18′S 36°55′E / 1.300°S 36.917°E / -1.300; 36.917