Enrique Iglesias (albamu)

Enrique Iglesias ni jina la kutaja albamu ya kwanza ya msanii wa muziki wa pop Enrique Iglesias. Albamu ilitolewa mnamo mwaka wa 1995. Albamu ilipata mafanikio kwa kiasi kikubwa na kushika nafasi za juu katika chati za Kilatini na pia ilirekodiwa kwa lugha ya Kireno[1] na Kiitalia. Albamu imejipatia Tuzo za Grammy kwa ajili ya Best Latin Pop Album kunako mwaka wa 1996.

Enrique Iglesias
Enrique Iglesias Cover
Studio album ya Enrique Iglesias
Imetolewa 21 Novemba 1995
Imerekodiwa 1995
Aina Latin, Pop, Soft Rock
Urefu 34:33
Lebo Fonovisa
Mtayarishaji Rafael Pérez-Botija
Tahakiki za kitaalamu
Wendo wa albamu za Enrique Iglesias
Enrique Iglesias
(1995)
Vivir
(1997)
Single za kutoka katika albamu ya Enrique Iglesias
  1. "Si Tú Te Vas"
    Imetolewa: 14 Oktoba 1995
  2. "Experiencia Religiosa"
    Imetolewa: Februari 1996
  3. "Por Amarte"
    Imetolewa: Mei 1996
  4. "Muñeca Cruel"
    Imetolewa: Julai 1996
  5. "No Llores Por Mí"
    Imetolewa: Agosti 1996
  6. "Trapecista"
    Imetolewa: Novemba 1996


Albamu ilijapatia Dhahabu katika thibitisho za Kireno baada ya majuma matano ya mauzo yake, na imeuza zaidi ya nakala milioni 8 kwa hesabu ya dunia nzima.[2] Huko Marekani ilitunukiwa dhahabu mnamo 11 Juni 1996 na kwenda katika ngazi ya platinumu mnamo 18 Novemba 1996,[3] na RIAA.

Vibao vinato kutoka katika albamu hii vimeshika nafasi ya kwanza kwenye chati za Billboard Hot Latin Tracks: "Si Tú Te Vas", "Experiencia Religiosa", "Por Amarte", "No Llores Por Mí" na "Trapecista", ni zaidi albamu yoyote ya Kilatini, imevunja rekodi ya awali iliyowekwa na kina Selena na Jon Secada wakiwa nafasi ya juu katika chati nne tofauti.

Kibao cha "Inventame" kilirekodiwa upya kunako mwaka wa 1999 na mtunzi wake bwana Marco Antonio Solís na kikaingizwa katika albamu ya Trozos de Mi Alma. Toleo hili limeshika nafasi ya 36 katika chati za Nyimbo za Kilatani.[4]

Orodha ya nyimbo hariri

  1. No Llores Por Mí (Enrique Iglesias/Roberto Morales) — 4:00
  2. Trapecista (Rafael Pérez-Botija) — 4:28
  3. Por Amarte (Enrique Iglesias/Roberto Morales) — 4:05
  4. Si Tú Te Vas (Enrique Iglesias/Roberto Morales) — 4:00
  5. Si Juras Regresar (Rafael Pérez-Botija) — 4:21
  6. Experiencia Religiosa (Chein García-Alonso) — 5:28
  7. Falta Tanto Amor (Enrique Iglesias/Roberto Morales) — 3:54
  8. Inalcanzable (Enrique Iglesias/Roberto Morales) — 3:34
  9. Muñeca Cruel (Rafael Pérez-Botija) — 4:20
  10. Invéntame (Marco Antonio Solís) — 3:50

Michakaliko katika chati hariri

Chati Nafasi iliyoshika
U.S. Billboard 200 148
US Billboard Top Latin Albums 1
US Billboard Latin Pop Albums 1
Mexican Top 100 Albums Chart 1
Dutch Albums Chart 67
Belgian Albums Chart (Flanders) 21
Spanish Top 100 Albums Chart 5

Tanbihi hariri

  1. ""Canta Em Portugues - Enrique Iglesias" on allmusic.com". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-06-25. Iliwekwa mnamo 2011-03-26.  Unknown parameter |= ignored (help) Archived 25 Juni 2011 at the Wayback Machine.
  2. ""Enrique Iglesias" on terra.com". Iliwekwa mnamo 2008-01-29. 
  3. ""Gold & Platinum Certifications" on riaa.com". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-01-05. Iliwekwa mnamo 1996-11-18. 
  4. ""Hot Latin Songs" on Billboard.com". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-01-31. Iliwekwa mnamo 2000-08-05.