Fanie Eloff, (jina lakuzaliwa Stephanus Johannes Paulus Eloff (1885-1947 )) alikua mtoto wa pili kuzaliwa wa Frederik Christoffel Eloff na Elsie Francina Eloff . Waliishi karibu na babu yake, Rais Paul Kruger wa Zuid Afrikaanse Republiek huko Pretoria.

Eloff pamoja na wasanii wengine mashuhuri wa Afrika Kusini kama Jacobus Hendrik Pierneef, Gerard Moerdijk na Gordon Leith walisomea Staats Model School huko Pretoria hadi kuzuka kwa Vita vya Anglo Boer (1899-1902). Familia ya Eloff ilimfuata Paul Kruger uhamishoni Uswizi baada ya kuanguka kwa Pretoria mnamo 3 Septemba 1900. Baada ya kifo cha Kruger mnamo 1904 akina Eloff walirudi Pretoria na Fanie Eloff kumalizia shule. Alijiunga katika Shule ya Migodi ya Afrika Kusini huko Johannesburg katika kozi ya jiolojia. [1]

Marejeo hariri

  1. De Kamper, Gerard & Chris de Klerk. Sculptured, The complete works of Fanie Eloff. University of Pretoria, 2011, p. 12
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fanie Eloff kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.