Fransisko Saveri ni jina la kawaida la Francisco de Jasso y Azpilicueta (Javier, Navarra, leo nchini Hispania, 7 Aprili 1506 - kisiwa cha Shangchuan, China, 3 Desemba 1552) alikuwa padri wa Shirika la Yesu, ambalo alichangia kulianzisha pamoja na Ignas wa Loyola.

Fransisko Saveri akimuongoa Paravas huko Goa, India, katika picha ya karne ya 19.
Safari zake.
Ngome ya familia ya Xavier.
"Njozi ya Mt. Fransisko SaverI", ilivyochorwa na Giovanni Battista Gaulli.
Kioo katika kanisa la Hong Kong kikimchora akimbatiza Mchina.
Kanisa la Saint-Pierre de Montmartre, Paris, alipoweka nadhiri zake.
Kaburi lake katika Basilika la Yesu Mwema huko Goa.

Baadaye alitangaza Injili katika nchi nyingi za Ulaya, Afrika na Asia hata akawa kati ya wamisionari maarufu zaidi ya historia ya Kanisa.

Alitangazwa na Papa Paulo V kuwa mwenye heri tarehe 25 Oktoba 1619, halafu Papa Gregori XV akamtangaza mtakatifu tarehe 12 Machi 1622.

Anaheshimiwa na Waanglikana na Walutheri pia.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[1]

Sala yake hariri

Ee Mungu wa mataifa yote ya dunia, uukumbuke umati wa Wapagani ambao, ingawa waliumbwa kwa sura yako, hawajakufahamu wewe wala kifo cha Mwanao Yesu Kristo, mwokozi wao.

Fanya kwamba, kwa sala na kazi za Kanisa lako takatifu, wakombolewe kutoka ushirikina wote na utovu wa imani wakaletwe kwenye ibada zako.

Kwa njia ya yule uliyemtuma awe ufufuo na uzima wa watu wote, huyo Mwanao Yesu Kristo, Bwana wetu.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

  • This article incorporates material from the Schaff-Herzog Encyclopedia of Religion
  • Attwater, Donald. (1965) A Dictionary of Saints. Penguin Books, Middlesex, England. Reprint: 1981.
  • Jou, Albert. (1984) The Saint on a Mission. Anand Press, Anand, India.

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.