Fudi
Fudi mwekundu (Foudia madagascariensis)
Fudi mwekundu (Foudia madagascariensis)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Passeroidea (Ndege kama shomoro)
Familia: Ploceidae (Ndege walio na mnasaba na kwera)
Jenasi: Foudia
Reichenbach, 1850
Ngazi za chini

Spishi 6:

Fudi (kutoka Kimalagasi: fody) ni ndege wadogo wa jenasi Foudia katika familia Ploceidae ambao wanatokea Madagaska na visiwa vingine katika Bahari ya Hindi. Ndege hawa ni wakubwa kuliko kwera na wakati wa kuzaa madume wana nyekundu au njano kichwani na pengine sehemu nyingine za mwili. Spishi nyingine hula mbegu hasa, nyingine hula wadudu hasa. Hulifuma tago lao kwa manyasi na majani na hulining'inizia kitawi au jani kubwa. Jike huyataga mayai 2-3.

Spishi hariri

Picha hariri

  Makala hii kuhusu "Fudi" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili fody kutoka lugha ya Kimalagasi. Neno (au maneno) la jaribio ni fudi.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.