Gambia, kirasmi Jamhuri ya Gambia, ni nchi ndogo kabisa ya Afrika bara. Eneo lake lote linazungukwa na Senegal kwa kufuata mwendo wa mto Gambia hadi Bahari ya Atlantiki.

Jamhuri ya Gambia
Republic of The Gambia (Kiingereza)
Kaulimbiu ya taifa:
Progress, Peace, and Prosperity (Kiingereza)
"Maendeleo, Amani, na Usitawi"
Wimbo wa taifa:
For The Gambia Our Homeland (Kiingereza)
"Kwa Gambia, Nchi Yetu"
Mahali pa Gambia
Mahali pa Gambia
Ramani ya Gambia
Ramani ya Gambia
Mji mkuuBanjul
13°28′ N 16°36′ W
Mji mkubwa nchiniSerekunda
13°26′ N 16°41′ W
Lugha rasmiKiingereza
Makabila (asilimia)[1]34.4 Wamandinka
24.1 Wafulani
14.8 Wawolof
10.5 Wajola
8.2 Wasoninke
3.1 Waserer
1.9 Wamanjago
1.3 Wabambara
0.5 Waaku
1.5 wengine
Dini (asilimia)[2]94.4 Waislamu
3.5 Wakristo
0.1 wengine
Eneo
 • Eneo la jumlakm2 11 300[3]
Idadi ya watu
 • Kadirio la 20232 468 569[3]

Kimsingi nchi yote ni maeneo ya kandokando ya mto huo; urefu ni takriban km 500, upana kati ya 10 na 50.

Historia hariri

Zamani eneo la Gambia lilikuwa sehemu ya Dola la Mali na Dola la Songhai.

Nchi kama ilivyo leo imepatikana kutokana na mvutano kati ya Uingereza na Ufaransa wakati wa ukoloni.

Mwanzoni Uingereza ulitafuta tu njia ya maji kwa ajili ya biashara, bila kujali utawala wa nchi.

Mapatano kati ya Ufaransa na Uingereza baada ya vita vya Napoleon Bonaparte yaliimarisha hali hiyo. Wafaransa walichukua eneo lote kubwa la Senegal, na Waingereza ile kanda ndogo ndani ya Senegal.

Tangu uhuru wa nchi zote mbili palikuwa na mpango wa kuziunganisha kwa njia ya shirikisho lililoanzishwa mwaka 1982 lakini Gambia ilitoka katika mapatano hayo mwaka 1989.

Hadi mwaka 1994 Gambia ilifuata mfumo wa demokrasia ya vyama vingi lakini mwaka ule uasi wa wanajeshi ulipindua serikali na kuwa chanzo cha utawala wa Yahya Jammeh aliyekuwa kiongozi, kwanza kama mwenyekiti wa kamati ya kijeshi, baadaye kama rais aliyechaguliwa mwaka 1996 na kuchaguliwa tena miaka 2001, 2006 na 2011. Isipokuwa mwaka 2001 wapinzani na watazamaji wa nje walilalamika ya kwamba kura hazikuwa huru.

Mwaka 2013 Jammeh alitoa Gambia katika Jumuiya ya Madola kama chombo cha ukoloni mamboleo.

Mwaka 2015 Jammeh alitangaza Gambia kuwa nchi ya Kiislamu.

Katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2016 vyama vya upinzani viliungana, na mgombea wao Adama Barrow alishinda, ilhali Jammeh awali alikubali kushindwa, lakini baada ya siku nane alitangaza ya kwamba alitaka kubatilisha matokeo na kuwa na uchaguzi mpya.[4]

Wananchi walianza kukimbilia nchini Senegal.

Tarehe 19 Januari 2017, rais mteule aliapishwa katika ubalozi wa Gambia huko Dakar, halafu wanajeshi wa Senegal, Nigeria na Ghana walivamia nchi ili kumuondoa madarakani kwa idhini ya Umoja wa Mataifa.

Tarehe 21 Januari Jammeh alikubali kuachia. Mwandamizi wake amerudisha nchi katika Jumuiya ya Madola.

Wakazi hariri

Wakazi wa nchi ni hasa wa kabila la Wamandinka, halafu Wafulani na Wawolof, jumla milioni 1.9 hivi.

Lugha rasmi ni Kiarabu, si tena Kiingereza (kuanzia mwaka 2016).

Upande wa dini, Uislamu unafuatwa na 90% za wakazi, Ukristo (hasa Kanisa Katoliki) na 8%, wakati wafuasi wa dini asilia za Kiafrika ni 2%.

Uchumi hariri

Uchumi unategemea kilimo, uvuvi na hasa utalii. Mwaka 2008, thuluthi moja ya wananchi hawakuwa na kipato cha $ 1.25 kwa siku.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. National Population Commission Secretariat (April 30, 2005). 2013 Population and Housing Census: Spatial Distribution. The Republic of The Gambia.
  2. The World Factbook: Gambia, The (en).
  3. 3.0 3.1 Gambia. The World Factbook. Central Intelligence Agency.
  4. Gambia: troops deployed to streets as president rejects election defeat theguardian.com 10-12-2016, imeangaliwa 10-12-2016

Marejeo hariri

  • Bennet, Lindsey and Voormeij, Lisa, The Gambia (Travellers), (Thomas Cook Publishing, 2009)
  • Emms, Craig and Barnett, Linda, Gambia (Bradt Travel Guides), (Bradt Travel Guides, 2006)
  • Hughes, Arnold, Historical Dictionary of the Gambia, (Scarecrow Press, 2008)
  • Hughes, Arnold and Perfect, David, A Political History of The Gambia, 1816–1994, (University of Rochester Press, 2008)
  • Gregg, Emma and Trillo, Richard, The Rough Guide to The Gambia, (Rough Guides, 2006)
  • Kane, Katharina, Lonely Planet Guide: The Gambia and Senegal, (Lonely Planet Publications, 2009)
  • Rice, Berkeley, Enter Gambia: The Birth of an Improbable Nation, (Houghton Mifflin. 1967)
  • Sarr, Samsudeen, Coup D'etat by the Gambia National Army, (Xlibris, Corp., 2007)
  • Sternfeldt, Ann-Britt, The Good Tourist in The Gambia: Travelguide for conscious tourists Translated from Swedish by Rolli Fölsch (Sexdrega,2000)
  • Tomkinson, Michael, Michael Tomkinson's Gambia, (Michael Tomkinson Publishing, 2001)
  • Various, Insight Guide: Gambia and Senegal, (APA Publications Pte Ltd., 2009)
  • Wright, Donald R, The World and a Very Small Place in Africa: A History of Glogalization in Niumi, The Gambia (New York: M.E. Sharpe, 2004)

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Serikali
Taarifa za jumla
Afya
Utalii
Biashara


Nchi za Afrika  
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Gambia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.