Gang Starr lilikuwa kundi la muziki wa hip hop lenye athira kubwa ya East Coast hip hop. Kundi linaunganisha watu wawili, ambao ni MC Guru na DJ/mtayarishaji DJ Premier. Kundi hilo lilijulikana sana kwa staili ya aina yao, ambayo inajumlisha baadhi ya elementi za hip hop na swing jazz ya New York.

Gang Starr
DJ Premier na Guru
Maelezo ya awali
Asili yake Boston, Massachusetts
Brooklyn, New York
Aina ya muziki Hip hop
Jazz rap
Alternative hip hop
Miaka ya kazi 1987 - 2005
Studio Wild Pitch
Chrysalis
Noo Trybe Records
Virgin
Ame/Wameshirikiana na Gang Starr Foundation
Wanachama wa zamani
Guru
DJ Premier
Gang Starr (1999)

Historia hariri

Kundi lilianzishwa mnamo mwaka wa 1986 na Guru (baadaye akaja kujulikana kama Keithy E. The Guru) na DJ 1,2 B-Down (pia anajulikana kama Mike Dee) na watayarishaji kadhaa, kama vile Donald D, J.V. Johnson au DJ Mark the 45 King naye alisaidia kuanzishwa kwa kundi hili. Mnamo 1987 na 1988, Gang Starr wakatoa single ya kwanza iliyofanyika katika studio za Wild Pitch label.

Mnamo 1989, kundi likasambaratika na wanachama pekee waliotaka kuliendeleza kundi wakapendekeza jina la Gang Starr, na huyo alikuwa Guru. Baadaye akapata kuwasiliana na DJ Premier (baadaye akajakujulikana kama Waxmaster C) ambaye alimtumia tepu ya biti iliyompendeza Guru. Baada ya kuipata biti, akaona bora amwalike DJ Premier ili aungane na Gang Starr na katika mwaka huohuo wakatoa single yao iliyokwenda kwa jina la "Words I Manifest" ikiwa sambamba na albamu iliyopewa jina la "No More Mr. Nice Guy" (1989).

Wakati wa shughuli zao Gang Starr walisaidia kuvumbua sauti ya hip hop ya New York. Matoleo yote ya Gang Starr, hasa Step in the Arena (1991), Daily Operation (1992) "Hard to Earn" (1994) na Moment of Truth (1998) zilipata heshima kubwa saana. Wimbo wa "Jazz Thing", uliokuwemo kwenye filamu ya Spike Lee ya Mo' Better Blues, ilisaidia kuinua sauti ya jazz rap.

Gang Starr Foundation hariri

Hali ya sasa hariri

Discografia hariri

  • No More Mr. Nice Guy
    • Imetolewa: 1989
    • Billboard 200 chati: -
    • R&B/Hip-Hop chati: 83
    • Mauzo ya U.S.: 53,000[1]
    • Single: "Words I Manifest"/"DJ Premier In Deep Concentration"/"Here's The Proof", "Positivity"/"No More Mr. Nice Guy (Remix)"
  • Step in the Arena
    • Imetolewa: 15 Januari 1991
    • Billboard 200 chati: 121
    • R&B/Hip-Hop chati: 19
    • Mauzo ya U.S.: 287,000[1]
    • Single: "Just To Get A Rep"/"Who's Gonna Take The Weight?", "Love Sick"/"What You Want This Time?"/"Credit Is Due", "Step In The Arena"/"Check The Technique (Remix)"/"Credit Is Due"
  • Daily Operation
    • Imetolewa: 5 Mei 1992
    • Billboard 200 chati: 65
    • R&B/Hip-Hop chati: 14
    • Mauzo ya U.S.: 297,000[1]
    • Single: "2 Deep"/"Take It Personal"/"Ex Girl to Next Girl"/"B.Y.S."/"Soliloquy of Chaos"
  • Hard to Earn
    • Imetolewa: 8 Machi 1994
    • Billboard 200 chati: 25
    • R&B/Hip-Hop chati: 2
    • Mauzo ya U.S.: 389,000[1]
    • Single: "Code of the Streets"/"Speak Ya Clout", "Dwyck", "Mass Appeal", "Suckas Need Bodyguards"/"The ? Remainz"/"Now You're Mine"
  • Moment of Truth
    • Imetolewa: 31 Machi 1998
    • Matunukio: Dhahabu
    • Billboard 200 chati: 6
    • R&B/Hip-Hop chati: 1
    • Mauzo ya U.S.: 500,000
    • Singles: "Royalty", "You Know My Steez"/"So Wassup?", "The Militia"/"You Know My Steez (Three Men And A Lady Remix)"
  • The Ownerz
    • Imetolewa: 24 Juni 2003
    • Billboard 200 chati: 18
    • R&B/Hip-Hop chati: 5
    • UK chati: 74
    • Mauzo ya U.S.: 191,000[1]
    • Single: "Skills"/"Natural", "Nice Girl, Wrong Place"/"Rite Where U Stand", "The Ownerz"/"Same Team, No Games"
  • Mass Appeal: Best of Gang Starr
    • Imetolewa: 26 Desemba 2006
    • Billboard 200 chati:
    • R&B/Hip-Hop chati:
    • Single:
  • Gang Starr appeared on the Brand New Heavies 1992 album "Heavy Rhyme Experience, Vol. 1 " with a track called "It's Gettin' Hectic"

Marejeo hariri

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 UKMIX - Forums - View topic - SoundScan Era - USA's Best Selling Artists and Albums. Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-06-21. Iliwekwa mnamo 2009-05-26.

Viungo vya Nje hariri