Geoffrey William Griffin

Dkt Geoffrey William Griffin (Eldoret 15 Juni 1933 - 28 Juni 2005) alikuwa mkurugenzi mwanzilishi wa Shule ya Upili ya Wavulana ya Starehe. Alianzisha shule hii mwezi Novemba 1959 kwa msaada wa marehemu Geoffrey Geturo na Joseph Gikubu, Afisa Mwandamizi wa sasa wa mkurugenzi wa shule; alikuwa Mkurugenzi wa shule hii kutoka alipo ianzilisha hadi mwisho wa maisha yake. Pia alikuwa mkurugenzi mwanzilishi wa National Youth Service kati ya 1964 na 1988, wakati alistaafu kutoka Huduma kwa Umma ya Kenya.

Starehe hutoa elimu ya hali ya juu bila malipo kwa mayatima na watoto wengi maskini wa Afrika (kwa mfumo unaofanana na Christ's Hospital). Wanfunzi wengi wa zamani sasa ni watu maarufu nchini Kenya na ulimwenguni. (Waziri mstaafu Raphael Tuju; Paul Ereng, mshindi wa medali ya dhahabu ya Olimpiki; Dk Amrose Misore, Naibu Mkuu wa Mkurugenzi wa Huduma ya Afya; na Prof George Magoha, Daktari wa upasuaji na Mwanaurolojia ambaye ni Makamu wa Chansela wa sasa wa Chuo Kikuu cha Nairobi ni wachache tu ya Wanastarehe wa zamani).

Ni vyema kutambua kwamba aliyeingia mahala pa Dkt Griffin kama Mkurugenzi wa Shule ya Upili ya Wavulana ya Starehe ni Prof Jesse Mugambi, muelimishaji aliyeheshimika na kujulikana sana nchini Kenya na awali alikuwa profesa wa falsafa katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Wana watatu wa Profesa Mugambi wamepitia katika Shule ya Starehe kama wanafunzi wakati tofauti wakati Dkt Geoffrey William Griffin bado alikuwa mkurugenzi. Profesa alijiuzulu kutoka wajibu wake kama Mkurugenzi wa Shule ya Starehe mnamo Ijumaa, 16 Januari 2009. Sababu iliyotolewa ya kujiuzulu ghafla kwake ilikuwa kwamba Chuo Kikuu cha Nairobi kilikataa kuongezea muda wa mkataba wake na kumtaka arejelee wajibu wake kama profesa wa falsafa.

Griffin alipata elimu isiyo ya juu sana: baada ya kuacha shule mapema, alijiunga, kwanza, na Usoroveya wa Kenya, na kisha King's African Rifles. Baada ya kutumikia wakati wa dharura, alikuja kushawishika na haki ya vuguvugu la Mau Mau, na kuchoshwa na ukatili wa vita.[1] Hakuendelea na tume yake, na alianza kushiriki katika jitihada za kukarabati wapiganaji wa zamani waliokamatwa, au walioachiliwa hivi karibuni kutoka kambi za uzuizi. Baada ya miaka kadhaa, aligeuza harakati zake kwa watoto waliofanywa yatima na vita, na kuanzishaa kituo cha kuwaokoa , kilichokua chanzo cha Starehe.

Griffin aliondokea kuwa kiongozi mwanzilishi kielimu na alituzwa PhD ya Heshima katika Elimu na Chuo Kikuu cha Kenyatta kwa kuifanya Shule ya Starehe kuwa mojawapo wa shule bora zaidi sio tu nchini Kenya bali katika Afrika na ambayo inajulikana ulimwengu mzima kama kituo cha ubora wa elimu.

Alipatiwa cheo cha Moran of the Order of Burning Spear na Rais Kenyatta mwaka wa 1970, ya Moran of the Order of the Golden Heart na Rais Moi mwaka wa 1986 na Order of the British Empire na Malkia Elizabeth II mwaka wa 2002, na tuzo ya Lifetime Achievement na Tume ya Kitaifa ya Kutetea Haki za Binadamu ya Kenya mwaka wa 2005 [1] Archived 27 Septemba 2007 at the Wayback Machine.

Vidokezo hariri

  1. [0] ^ Anonymous ( 18 Agosti 2005) The Times of London online obituary.

Makala ya Waandishi hariri

  • Geoffrey Griffin (1994) School Mastery: Straight talk about boarding school management in Kenya, (Nairobi: Lectern Publications).
  • Roger Martin (1978) Anthem of bugles: the story of Starehe Boys Centre and School, (Nairobi, London: Heinemann Educational).
  • Kennedy OA Hongo, Jesse NK Mugambi (2000) Starehe Boys Centre: School and Institute .first forty years 1959-1999 (Nairobi: Acton Publishers)

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Geoffrey William Griffin kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.