Gordon MacKenzie Gilbert (alizaliwa 1982) ni mchezaji wa soka wa Scotland na Afrika Kusini ambaye alicheza kama beki wa kushoto au beki wa kati katika Ligi Kuu ya Soka ya Afrika Kusini.

Alianza maisha yake ya soka akiwa St. Johnstone huko Scotland na baadaye aliichezea East Fife katika ligi ya scotland huku akiisaidia timu iyo kupanda daraja kufikia daraja la pili. Baadaye, Gilbert alihama Afrika Kusini na kucheza katika Timu ya FC ya Tuks na Mpumalanga Black Aces, ambapo alifanikiwa kufika fainali ya Kombe la Nedbank na Black Aces.

Kutokana na uchezaji wake thabiti Gordon alichaguliwa kujiunga na Timu ya Taifa ya Maendeleo ya Afrika Kusini. Mwaka 2008, alijiunga na Kaizer Chiefs na akashinda mashindano kadhaa nao kabla ya kwenda kwa mkopo kwa Moroka Swallows. Mwaka 2013, Gilbert alisaini mkataba na Thanda Royal Zulu FC.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gordon Gilbert kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.