Inpop Records ni kampuni ya kurekodi muziki ya kisasa ya Kikristo iliyokuwa na makao yake Franklin,Tennessee,Marekani.Ilianzishwa mnamo mwaka wa 1999 na Waaustralia Peter Furler na Wes Campbell. Jina laolilitokana na wazo la kutaka kuonyesha talanta ya wasanii wa kimataifa katika aina ya muziki ya pop, ingawaje wana mikataba na wanamuziki wa Marekani pia. Wasanii wanaorekodi nyimbo na Inpop wanahusisha Newsboys, Mat Kearney, Everyday Sunday,na Superchick.

Inpop Records
Shina la studio Sony Music Entertainment
Imeanzishwa 1999
Mwanzilishi Peter Furler, Wes Campbell
Nchi MarekaniMarekani
Mahala Franklin, Tennessee
Tovuti www.inpop.com

Historia hariri

Mwanamuziki kiongozi wa Newsboys,Peter Furler na Meneja wa bendi,Wes Campbell, walipowasili Marekani kwa mara ya kwanza(katika miaka ya 1980), hawakuwa na nia yoyote ya kumiliki kampuni ya kurekodi muziki. Mwongo mmoja baadaye,Furler aliamua kuwa amechoka kuishi na mamia ya nyimbo za wasanii katika basi yake,nyimbo hizo alikuwa amepewa na wanamuziki wadogowadogo katika ziara yake. Hapo ndipo akaamua kufanya jambo la kutatua shida hiyo, yeye na Campbell wakaanzisha Inpop Records. Lengo la Inpop likawa kuvumbua wanamuziki bora duniani wanaoelewa neema ya injili ya Yesu Kristo na wana muziki mpya na tofauti ya Kikristo.

"Katika safari yetu duniani,tumeona maelfu ya mabendi na wasanii Tuna wito tunaotoa kwa wanamuziki ya kupa wasanii hawa fursa sawa na yenye Newsboys walipewa, " alisema Furler.

Wasanii wa Inpop hariri

Newsboys ndio wasanii wa Inpop wanaojulikana sana. Kiongozi wa kikundi hiki ni mwimbaji,Peter Furler, mwnachama wa Bethel na Campbell ndio meneja wa kundi. Wakati mmoja,tovuti ya Newsboys ilikuwa na kiungo cha tovuti ambapo watu wangeweza kununua Biblical Foundations,kitabu cha kujifunza kuhusu Biblia kilichochapishwa na Broocks na Murrell. Kitabu hicho kinajulikana kwa jina maarufu The Purple Book. Kiungo hicho kinauliza swali, "Je, umefanya The Purple Book?" Pia,katika tovuti kuna barua kutoka Furler inayoeleza jinsi "kufanya The Purple Book" ilimbadilisha. Funzo la kila siku kutoka Laffoon lilipewa nafasi katika tovuti yao.[1] Hadi sasa bado kuna kiungo cha mafuzo ya Laffoon katika tovuti yao.

Wasanii wa hapo awali wa Inpop hariri

  • Bob Smiley (Marekani) (Bado apo kazini)
  • Beanbag (bendi) (Australia) (Liliacha kuimba)
  • Casting Pearls (Marekani) (Walibadilisha jina kuwa VOTA, hivi sasa wanarekodi na INO Records)
  • Charmaine (Australia) (Aliacha kuimba)
  • Fusebox (bendi) (Marekani)
  • Go Fish (Christian band) (Marekani) (Bado anaimba, muziki ya watoto)
  • Foolish Things (Marekani) (Liliacha kuimba)
  • Ian Eskelin (Marekani) (Bado anaimba)
  • Petra (bendi) (Marekani) (Liliacha kuimba)
  • Phil Joel (New Zealand) (Anaimba, anarekodi na deliberatePeople Records)
  • Plus One (bendi) (Marekani) (Liliacha kuimba)
  • Sarah Brendel (Ujerumani) (Bado anaimba)
  • Tree63 (Afrika Kusini) (Liliacha kuimba)

Inpop Records,pia, ndio wanaoendesha tukio la kila mwaka liitwalo Festival Con Dios.

Angalia Pia hariri

Viungo vya nje hariri

Marejeo hariri