Isaya III ni jina lililobuniwa na wataalamu wa Biblia ili kumtaja mwandishi asiyejulikana wa sura 56-66 za kitabu cha Isaya, ingawa wengine wanadhani ni waandishi zaidi ya mmoja.

Sura hizo zinakadiriwa kuwa ziliandikwa baada ya uhamisho wa Babeli (500 hivi K.K.) na zinawakaribisha watu wa mataifa yote kujiunga na Israeli katika kumuabudu Mungu pekee.

Kiini chake ni 61:1-3.

Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Isaya III kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.