James Cook (tamka: jems kuk; * Uingereza, 27 Oktoba 1728Hawaiʻi, 14 Februari 1779) alikuwa nahodha, mpelelezi na mchoraji wa ramani Mwingereza katika karne ya 18.

Captain James Cook mnamo 1775 alivyochorwa na Nathaniel Dance

Amejulikana hasa kutokana safari tatu katika Bahari ya Pasifiki na taarifa zake juu ya safari hizi. Cook alitembelea visiwa vingi visivyojulikana Ulaya hadi wakati ule akivipima na kuvichora kwenye ramani za Ulaya kwa mara ya kwanza.

Alizunguka dunia yote mara mbili. Kati ya maeneo aliyoyaweka kwenye ramani za dunia ni pwani la mashariki ya Australia, visiwa vya Hawaii, Newfoundland na New Zealand. Alivuka Mzingo wa Antaktiki na kupata kuona visiwa vipya na mandhari huko Amerika ya Kaskazini na Pasifiki ya Kusini.

Yeye ni maarufu kwa kutafuta pwani ya mashariki ya Australia, kuviona Visiwa vya Hawaii na ramani ya kwanza ya Newfoundland na New Zealand. Ndiyo sababu anaitwa "mtafiti wa Uingereza".

Wakati wa safari zake, alitumia muda mwingi juu ya majaribio ya sayansi, na ramani za maeneo mapya. Pia aliandika vitabu vingi kuhusu kile alichokiona.

Cook aliuawa na wenyeji wa Hawaii alipotembelea kisiwa mara ya tatu.

Visiwa vya Cook hutunza kumbukumbu ya jina lake.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu James Cook kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.