James Omingo Magara

James Omingo Magara ni mwanasiasa wa Kenya. Kwa sasa ni mwanachama wa Orange Democratic Movement na alichaguliwa kuwa mbunge wa Mugirango Kusini katika uchaguzi wa 2007.

James O. Magara

Alishinda kiti hiki mara ya kwanza kwa tiketi ya FORD-Kenya katika uchaguzi mdogo mnamo 2001, akichukua nafasi ya nduguye Enock Nyakieya Magara aliyefariki katika ajali ya gari.

Alihifadhi kiti chake katika Uchaguzi mkuu wa Kenya wa 2002, wakati huu akiwakilisha chama cha Ford People na pia katika Uchaguzi wa 2007, akiwakilisha Chama cha ODM[1]

Uwaziri hariri

Tangu kuchaguliwa amewahi kuwa Naibu wa Waziri wa biashara. Hata hivyo, mnamo Desemba,2009, Mahakama kuu ya Kenya ilitangaza kiti cha Ubunge cha Mugirango Kusini wazi kutokana na udanganyifu katika uchaguzi, ingawa Magara mwenyewe hakupatikana na hatia ya udanganyifu[2]

Marejeo hariri

  1. Wabunge wa Bunge la 10 Archived 17 Juni 2008 at the Wayback Machine.. Bunge la Kenya, lililopatikana 19 Juni 2008
  2. Daily Nation, 17 Desemba 2009: Magara Apoteza Kiti cha Mugirango Kusini