Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kimoldova

Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kimoldova ilikuwa kati ya jamhuri wanachama 15 za Umoja wa Kisovyeti hadi 1991. Jina lake liliandikwa kwa Kikirili "Република Советикэ Сочиалистэ Молдовеняскэ (republika sovyetike sotsialiste moldovenyaske) au kwa maandiko ya Kilatini: Republica Sovietică Socialistă Moldovenească; kwa Kirusi: Молдавская Советская Социалистическая Республика.

Bendera ya Moldova ya Kisovyeti
Mahali pa Moldova katika Umoja wa Kisovyieti

Iliundwa 1940 kutokana maeneo mawili:

Wakazi wa sehemu hii ni hasa Waromania lakini kuna mchanganyiko na Warusi na Waukraine pia.

Wakati wa kuachana kwa Umoja wa Kisovyeti jina likabadilishwa kuwa Jamhuri ya Moldava lililotangaza uhuru wake 27 Agosti 1991 kuwa Moldova.