Jens Stoltenberg (amezaliwa 16 Machi 1959) ni mwanasiasa wa Norwei. Alikuwa Waziri Mkuu wa Norwei kwanza tangu Machi 2000 mpaka Oktoba 2001, halafu tena kati ya Oktoba 2005 na Oktoba 2013. Tangu Oktoba 2014, yeye ni Katibu Mkuu wa NATO.

Jens Stoltenberg.

Yeye ni mbunge kutoka Oslo tangu mwaka 1993, na ni kiongozi wa Arbeiderpartiet (Chama cha Wafanyakazi) tangu mwaka 2002. Kabla ya Stoltenberg Waziri Mkuu wa Norwei alikuwa Kjell Magne Bondevik.