Johnson Sululu (amezaliwa tar. 26 Julai 1986) ni mtayarishaji, Dj na msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania. Anafahamika zaidi kwa jina la kitayarishaji kama Jors Bless au Dj.Jors Bless .

Jors Bless (Dj Jors Bless)
Jors Bless mwaka 2009
Jors Bless mwaka 2009
Jina Kamili {{{jina kamili}}}
Jina la kisanii Jors bless (Dj Jors Bless)
Nchi Tanzania
Alizaliwa 26 Julai 1986
Aina ya muziki Hip hip, Rnb , Afro pop & Tz urban music
Kazi yake Mtayarishaji, Dj, Msanii
Miaka ya kazi 2004 - hadi leo
Kampuni Sababisha records

Anafanya kazi katika studio ya Sababisha Records na ni mmiliki wa studio hiyo iliyopo jijini Dar na yupo tangu mwaka wa 2004 pale studio ilipoanzishwa. Bless amewahi kufanya kazi na wasanii kadhaa wa Bongo, kama vile Zola D, Mapacha, Joe Makini, Adili, Black, Kanyama, Rama D, Linex na Danny Msimamo, Niki wa pili,G nacko

Pia amewahi kufanya kazi katika studio mbali mbali nyinginge ikwemo studio iliyofahamika zaidi kwa kutengeneza muziki wa hip hop tanzania Pasu kwa Pasu ambako ndiko alikoanzia kazi ya utayarishaji wa muziki kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 18 tu ambako alipelekwa na wasanii Mapacha 50-50 baada ya kupata kusikia baadhi ya midundo yake aliyokuwa akiitengezea nyumbani, Jors bless anasema kufanya kazi pasu kwa pasu studios ndiko kulikomfungulia milango mingi ya ndoto zake za kufanya muziki kwani alipata nafasi ya kukutana na watu mbali mbali ambao walionyesha kukubali kazi zake na kumpa moyo akiwemo mtayarishaji mkongwe wa muziki Professor Ludigo ambaye hadi sasa wanafanya kazi pamoja katika studio za Sababisha Records.

Wasifu hariri

Maisha ya awali hariri

Muziki hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Afrika bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jors Bless kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.