Juma kuu (kwa Kilatini: Hebdomas Maior, lakini kwa kawaida zaidi Hebdomas Sancta yaani "Wiki Takatifu"; kwa Kigiriki: Ἁγία καὶ Μεγάλη Ἑβδομάς, Hagia kai Megale Hebdomas, "Juma Takatifu na Kuu") ni juma la mwaka ambalo Wakristo wanaadhimisha kwa namna ya pekee matukio makuu ya historia ya wokovu kadiri ya imani yao, kuhusiana na mwisho wa maisha ya Yesu huko Yerusalemu, uliofuatwa na ufufuko wake.

Yesu kuingia Yerusalemu kwa shangwe kwenye Jumapili ya Matawi ndio mwanzo wa Juma kuu.
Mwaka wa liturujia
Magharibi
Mashariki

Katika madhehebu mengi ya Ukristo, juma hilo linaanza na Jumapili ya matawi ambapo linaadhimishwa kwa shangwe tukio la Yesu Kristo kuingia huo mji mtakatifu kama mfalme wa Wayahudi huku akipanda punda na kushangiliwa na umati wa wafuasi wake, waliofurahia hasa alivyomfufua Lazaro wa Betania.

Lakini Yesu alieleza kuwa ufalme wake si wa dunia hii, na kuwa yeye hakuja kutumikiwa bali kutumikia na kutoa uhai wake uwe fidia ya umati.

Hivyo siku zilizofuata, hasa Ijumaa Kuu, alikabili kwa hiari mateso na kifo kutoka kwa wapinzani wake waliopitia mamlaka ya liwali Ponsio Pilato ili apewe adhabu ya kifo kwa kusulubiwa, na hatimaye akafufuka mtukufu usiku wa kuamkia Jumapili.

Kabla ya hapo Yesu alijumlisha hayo matukio yajayo katika karamu ya mwisho aliyokula pamoja na mitume wake 12, akiwaachia agizo la kufanya daima karamu ya namna hiyo kama ukumbusho wake.

Maandamano ya Ijumaa Kuu huko Ekwador.

Basi, kuanzia Alhamisi kuu jioni hadi Jumapili ya Pasaka jioni Wakristo[1] wanaadhimisha siku tatu kuu za Pasaka, zinazofanya ukumbusho wa Yesu mteswa, mzikwa na mfufuka[2][3] kama ifuatavyo:

  • Alhamisi kuu jioni hadi Ijumaa kuu jioni: siku ya Kristo mteswa
  • Ijumaa kuu jioni hadi Jumamosi kuu jioni: siku ya Kristo mzikwa
  • Jumamosi kuu jioni hadi Jumapili ya Pasaka jioni: siku ya Kristo mfufuka.

Kuhusiana na Pasaka ya Kiyahudi, ni lazima Juma kuu litokee mwishoni mwa Machi au kabla ya wiki ya mwisho ya Aprili.

Ushahidi wa kwanza kuhusu ibada za pekee za Wakristo wakati huo unapatikana katika "Katiba za Mitume" (kwa Kiingereza: "Apostolical Constitutions", 18, 19), zilizoandikwa katika nusu ya pili ya karne ya 3 hadi karne ya 4. Humo ulaji wa nyama unakatazwa wiki nzima, na mfungo kamili unaagizwa kwa siku za Ijumaa na Jumamosi Kuu.

Barua ya Denis wa Aleksandria (260 BK) inaonyesha taratibu hizo zimeshakuwa desturi.[4]

Tanbihi hariri

  1. Ramshaw, Gail (2004). The Three-Day Feast: Maundy Thursday, Good Friday, and Easter. Augsburg Books. p. 7. ISBN 9780806651156. Retrieved 13 April 2014. Many Christians are already familiar with the ancient, and now recently restored, liturgies of the Three Days: Maundy Thursday, Good Friday, and the great Easter Vigil service of light, readings, baptism, and communion. The worship resources published by the Evangelical Lutheran Church in America, the Episcopal Church, the United Methodist Church, the Presbyterian Church U.S.A. and the Roman Catholic Church include nearly identical versions of these liturgies. 
  2. Cooper, J.C. (23 October 2013). Dictionary of Christianity. Routledge. p. 124. ISBN 9781134265466. Retrieved 25 April 2014. Holy Week. The last week in LENT. It begins on PALM SUNDAY; the fourth day is called SPY WEDNESDAY; the fifth is MAUNDY THURSDAY; the sixth is GOOD FRIDAY; and the last 'Holy Saturday', or the 'Great Sabbath'. 
  3. Brewer, Ebenezer Cobham (1896). The Historic Notebook: With an Appendix of Battles. J. B. Lippincott. p. 669. Retrieved 25 April 2014. The last seven days of this period constitute Holy Week. The first day of Holy Week is Palm Sunday, the fourth day is Spy Wednesday, the fifth Maundy Thursday, the sixth Good Friday, and the last Holy Saturday or the Great Sabbath. 
  4. Apostolical Constitutions v. 18, 19

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Juma kuu kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.